01 August 2013

REDD'S MISS ILALA WAANZA MAZOEZI



Na Ester Maongezi
WANYANGE 15 kutoka katika vitongoji vinne vya Wilaya ya Ilala, wameanza mazoezi ya kumsaka mrembo wa Redd's Miss Ilala 2013 yanayofanyika katika Ukumbi wa klabu Billicanas uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo, Juma Mabakila, alisema mashindano hayo yanatarajia kufanyika Agosti 16, mwaka huu katika Ukumbi wa Golden Jubilee Tower, ambapo warembo watatu watakaoshika nafasi za juu watashiriki Redd's Miss Tanzania 2013.
Mabakila alisema warembo hao wanatoka katika vitongoji vya Mzizima, Tabata, Ukonga na Dar City Centre.Al i s ema ma a n d a l i z i y a mashindano hayo, yanaendelea vizuri na wamepania kuonesha vipaji vyao katika mchuano utakaofanyika wiki ijayo.
"Sisi kama kamati tunawaomba wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia muonekano mpya wa mashindano ya urembo, lakini pia kuangalia jinsi Ilala ilivyosheheni warembo watakaoleta ushindani mkubwa Redd's Miss Tanzania 2013," alisema.
Aliwataja warembo waliopo katika kambi ya Miss Ilala ni Alice Isaac, Clara Poul, Anna Johnson, Iren Mwelolo, Munira Mabrouk, Rehema Mpanda, Shamim Mohamed, Martha Gewe, Diana Joackim, Natasha Mohamed, Dorice Mollel, Pendo Lema, Kazumbe Mussa na Kabula Kibogoti.Alisema hadi sasa kampuni zilizojitokeza kuwadhamini ni Redd's, Dodoma Wine, CXC Tours, Chilly Will, Clouds FM, City Lounge, Times FM na Lemutuz Blog.

No comments:

Post a Comment