20 August 2013

TAMBWE ATUA DAR,KUIFUATA TIMU KAHAMA Na Amina Athumani
MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Simba, Hamis Tambwe kutoka Vital 'O ya Burundi amewasili nchini jana kwa ajili ya kujiunga na wekundu hao wa msimbazi.Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang'are alisema mchezaji huyo aliwasili jana kwa ajili ya kuichezea timu hiyo katika msimu huu wa ligi kuu.

Alisema mara baada ya kuwasili tayari Simba imeshakamilisha taratibu zote za mchezaji huyo kuichezea timu hiyo.Alisema mchezaji huyo ataondoka na kwenda Kahama, Shinyanga kujiunga na kikosi cha timu hiyo kilichoweka kambi ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kuanza kwa mechi zake za ligi kuu.
Alisema wachezaji wote waliosajiliwa na klabu yake watacheza katika ligi hiyo licha ya kuwepo kwa baadhi ya kasoro katika usajili wao.Aliwataja wachezaji hao ambao usajili wao ulikuwa na kasoro ndogondogo ni Betram Mombeki, ambaye amesema yupo tayari kuichezea Simba kwa kuwa hakuna klabu iliyomuwekea pingamizi licha ya kuwepo kwa taarifa zisizo rasmi za uwepo wa pingamizi.
Simba pamoja na klabu nyingine 13 za ligi kuu zipo katika maandalizi ya ligi hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi Jumamosi wiki hii. i.  

No comments:

Post a Comment