20 August 2013

KLINIKI YA THABEET YAFUTWA



 Na Mosi Mrisho
KLINIKI ya mchezo wa kikapu ya Hasheem Thabeet imefutwa kwa mwaka huu na Chama cha Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF),kutokana na mchezaji huyo wa NBA kuitwa na klabu yake huko Marekani kwenda kwenye ratiba maalum.

Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu Msaidizi wa TBF Michael Maluwe, alisema kliniki hiyo imefutwa kwa mwaka huu kwa sababu Hasheem Thabeet ameitwa na klabu yake kwenye ratiba yao maalum.
"Tumepata taarifa kutoka kwa uongozi wa Hasheem Thabeet kuwa anatakiwa kurudi nchini kwao mara moja kwenda kuendelea na ratiba yao ya kuhudhuria katika ligi kuu,"alisema Maluwe.
Maluwe alisema baada ya kumaliza ratiba hiyo ataelekea Afrika Kusini kuhudhuria Mafunzo ya Vijana wa Afrika maarufu kama Basketball Without Border (BWB).
Al i s ema ma f u n z o h a y o anayokwenda kuhudhuria yapo chini ya NBA Afrika na wachezaji wote watakaocheza katika ligi kuu ya NBA wanahitajika.
Maluwe aliongeza kuwa kliniki hiyo ilipangwa kufanyika jijini Arusha, ambapo mikoa zaidi ya mitano ilitakiwa kushiriki ikiwemo Dar es Salaam,Kilimanjaro,Dodoma na visiwa vya Zanzibar.
Kliniki hiyo ambayo hufanyika kila mwaka, mwaka huu ilipangwa kufanyika Agosti 16 hadi 18 jijini Arusha na kushirikisha vijana wasiopungua 200  

No comments:

Post a Comment