19 August 2013

SIRI YA MAUAJI MARA YAFICHUKA



Na Timothy Itembe, Mara
IMEELEZWA kuwa matukio ya ukatili mkoani Mara yanachangiwa na imani za kishirikina, kuvamia mali, ulevi, wivu wa kimapenzi na kulipiza kisasi pamoja na kukwepa mkondo wa sheria. Akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa waandishi wa habari na wadau wa maendeleo Mjini Musoma, Kamanda wa Polisi Mkoa Mara, Friednand Elyas alisema kuwa vitendo hivyo vinaongezeka kutokana na jamii kukosa elimu.

Aidha Elyas alisema kuwa kutokana na vitendo hivyo kuongezeka kila mwaka Jeshi la Polisi limeunda kikosi maalumu cha kupambana na kuzuia mauaji. "Jeshi la Polisi kwa kulitazama h i l i t ume amu a k u u n d a kikosi maalumu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mauaji, vipigo yanadhibitiwa na kimesaidia kuzuia mauaji," alisema Elyas.
Kamanda Elyas aliongeza kuwa kikosi hicho kitafanya kazi yake kwa njia ya kutoa elimu juu ya madhara ambayo yanaipata jamii punde matukio hayo yanapotokea ambayo y a n a c h a n g i a k u r u d i s h a nyuma harakati za kujiletea maendeleo.
Aidha wadau walipendekeza kuwa kuwepo njia bora ya kupashana habari baina ya wanahabari na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuondoa kero na usumbufu ambao unawapata waandishi wa habari katika kuandika na kutoa habari.
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mara (MRPC), Emanueli Bwimbo alisema kuwa waandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kunyimwa habari na baadhi ya viongozi wa mamlaka husika. Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa, Joseph Makinga alisema kuwa waandishi wa habari ni nguzo muhimu ya maendeleo hivyo wanapaswa kupewa ushirikiano.

No comments:

Post a Comment