27 August 2013

SHERIA YA VYAMA VYA USHIRIKA HAIKIDHI VIWANGO - CHIZANa Grace Ndossa
WAZIRI wa Kilimo Chakula na Ushirika Christopher Ch i z a a n awa s i l i s h a mswada wa sheria ya vyama vya ushirika Bungeni kesho kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya pili.Akizungumza hivi karibuni alisema kuwa mswada huo utasaidia kurekebisha sheria ya vyama vya ushirika pamoja na kuundwa kwa Tume ya kusimamia vyama hivyo ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Alisema kuwa mswada wa sheria hiyo mpya ya mwaka 2013 azma yake ni kufufua vyama vya ushirika pamoja na kuweka mazingira stahiki kwa wanachama na kuwepo kwa uongozi ambao unawajibika kwa wanachama.
"Kutungwa kwa sheria mpya ya mwaka 2013 ambao mswada huo utasomwa kwa mara ya pili katika kikao cha 11 cha bunge azma yake kubwa ni kufufua vyama vya ushirika pamoja na kuwepo kwa uongozi imara ambao wanachama watakuwa na imani nao," alisema Chiza.
Alisema kuwa sheria ya vyama vya ushirika iliyopo kwa sasa haikidhi viwango na imepelekea vyama vingi vya ushirika kufa na wanachama wamekosa imani navyo kutokana na ubadhirifu mkubwa kwenye vyama hivyo.
Al i o n g e z a k uwa s h e r i a inayotumika ni ya mwaka 2003 kutokana na mabadiliko ya kiuchumi kuna vipengele ambavyo vimepitwa na wakati, hivyo sheria hii mpya ya mwaka 2013 itasaidia kuondoa upungufu uliokuwepo.
Pia alisema kutakuwepo kwa tume itakayojitegemea na itapata ruzuku kutoka serikalini kwa ajili ya kuhakikisha vyama vya ushirika vinafanya kazi ipasavyo na kuondoa malalamiko yaliyokuwepo kwa wanachama.
Hata hivyo alisema sheria iliyopo haitoi adhabu ya kutosha kwa wanaohusika na ubadhirifu wa fedha ndiyo maana walipitia vipengele hivyo na kuvifanyia marekebisho ili iweze kutumika.
Alisema kuwa katika sheria hiyo pia walipendekeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kukagua mahesabu ya vyama vya ushirika ili kudhibiti ubadhirifu huo kwa vyama vya ushirika.

No comments:

Post a Comment