Na Pendo
Mtibuche, Dodoma
RIPOTI ya utafiti wa hali ya ukatili
nchini kwa kipindi cha mwaka 2010 inaonyesha kuwa theluthi moja ya wanawake
wote Tanzania
wameathirika kwa namna moja au nyingne na ukatili wa kijinsia tangu wakiwa na
umri wa miaka 15.Hali hiyo pia inaonyesha kuwa wanawake
hao hao pia wameathirika na vitendo vya ukatili katika kipindi cha miezi 12
iliyopita.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo y
a
siku mbili kwa viongozi mbalimbali wa dini, Serikali na watumishi wa idara
mbalimbali katika wilaya ya Bahi mkoani hapa juu ya mbinu za kuzuia ukali,
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutosha Shirika la Women, Wake Up (WOWAP) chini la
mradi wa tunaweza unaofadhiliwa na OXFAM Canada, Nasra Suleimani alibainisha
hayo.
Alibainisha kuwa ukatili huo unaonekana
kufanywa zaidi kwa wanawake waliotalikiwa, waliotengana na wenza wao au wajane.Nasra alisema kuwa takwimu zinaonyesha
kuwa mwanamke mmoja kati ya watano amewahi kufanyiwa ukatili wa kingono huku
asilimia kumi ya wanawake inaonyesha walifanya mapenzi kwa kulazimishwa yaani
bila idhini yao.
Al i s ema k uwa l e n g o l a
kuanzishwa kwa mradi huo wa tunaweza ni kuweza kupunguza hali ya watu kukubali
ukatili na kuona kwamba ni jambo la kawaida kumfanyia mwanamke vitendo ambavyo
kimsingi ni ukatili.Aidha alisema kwamba kampeni hiyo
itawezekana kwa kujenga umma unaopinga ukatili dhidi ya wanawake dhidi ya ya
ukatili na kushawishi jamii uacha vitendo hivyo.
Hata hivyo, alisema kuwa vitendo hivyo
vinaonekana kushamiri kutokana na kuwepo kwa tabia ya baadhi ya watu kuwa na
mtazamo wa jamii kuwa ni halali mwanamke kupigwa.Vilevile alisema kuwa tatizo lingine la
kuendelea kuenea kwa ukatili kunatokana na wanawake wenyewe kuona ni haki
kupigwa wanapokuwa wamefanya kosa.
Alisema kuwa wao kama wao wanajitahi
kutoa elimu kwa jamii kwa kuwaelimisha wananchi kutumia mbinu mbalimbali ili
waepukane na ukatili huo.Miongoni
mwa mbinu hizo ni pamoja na kuhamasisha mtu mmoja mmoja kubadili tabia zao juu
ya ukatili na kujenga washirika, kujenga muonekano wa kampeni kupitia mbinu
mbalimbali
No comments:
Post a Comment