23 August 2013

RIPOTI MAALUM:UBAKAJI WAJANE

  • UBAKAJI ULIOHALALISHWA HUFANYIKA MBELE YA MASHUHUDA


Bi. Arodia Gebasaki ambaye ni mjane akisimulia jinsi mila ya kutakasa wajane inavyofanyika kwa mwandishi wa makala haya (hayupo pichani) ambapo yeye alikataa kufanyiwa mila hiyo na hakuna madhara yoyote aliyopata tangu kufiwa na mume wake, miaka 14 iliyopita

Baadhi ya wajane wakiwa katika picha ya pamoja na mwandishi wa makala haya baada ya kufanya mahojiano kuhusu mila ya kutakasa wajane wilayani Ukerewe, Mwanza. Wajane hao wameipiga vita mila hiyo kutokana na kumdhalilisha mwanamke.
MWANDISHI Reuben Kagaruki

"Udhalilishaji huu uliojificha katika mila inayoitwa Okusomboka kwa Wakerewe ni tendo ambalo hufanyika kwa maana ya kuhitimisha uhusiano wa ndoa kati ya mume na mke aliyefiwa. Mila hiyo huhitaji uhusiano huo uhitimiswe hivyo sababu ulianzishwa kwa tendo la ndoa.BIBI a l i b a kwa , mama akabakwa, dada amebakwa na mke wangu atabakwa nitakapofariki.”


Huo ndiyo uhalifu mkubwa uliojificha kwenye mila ya Okusomboka (kutakasa) kwa wakazi wa Ukerewe hasa kwa Wakara na Wajita.Kwa Wakerewe ubakaji ni jambo la kawaida na unatukuzwa kwa mikono miwili kupitia mila ya Okusombaka.

Hayo ndiyo maisha ya kawaida kwa wakazi wa Ukerewe mkoani Mwanza wanaotukuza ubakaji, mbakaji anapomaliza tendo hilo, wakati mwingine anashangiliwa kwa kupigiwa vigelegele na akina mama akionekana shujaa wa kuondoa watu mikosi kupitia ubakaji, ingawa wao hutafsiri kuwa wanasomboka.

Ubakaji huo kupitia mila ya Okusomboka ni sehemu ya maisha ya kawaida kwa wakazi wa Ukerewe na unaheshimiwa kiasi kwamba wale wanaokataa kubakwa wanatengwa na kunyooshewa vidole kila wanapopita.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza juu ya mila ya Okusomboka (utakasaji) umebainisha vitendo vya ubakaji vimekuwa vikitendeka tangu enzi na enzi na kuingia katika karne hii ya sayansi na teknolojia.

Ambapo ubakaji huo, unalenga wanawake wajane na unafanyika siku ya nne ya matanga tangu kutokea kifo cha mwanaume ndani ya familia.Bila kujali uchungu anaokuwa nao mjane wa kupoteza mume wake, anatafutiwa mbakaji (Omwesya-yaani mtakasaji) ambaye anakodiwa na kulipwa ujira ili kutekeleza kitendo hicho cha kubaka mjane, ambacho kwa Ukerewe ni cha heshima, katika kuhitimisha uhusiano kati ya mume aliyekufa na mjane aliyebaki.

Ingawa sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya Mwaka 1998 inatoa adhabu kali kwa watu wanaopatikana na hatia ya makosa ya ubakaji, kwa Ukerewe hawajui kama Okusomboka ni kubaka, hivyo kukiuka wazi wazi sheria hiyo inayotolewa kwa watu wanaofanya vitendo hivyo.

Ubakaji unafanyika kwa uwazi na wameenda mbele zaidi kwani kuna watu maalumu ambao wanalipwa fedha na wakati mwingine hata mifugo kwa ajili ya kuwabaka wanawake wanaofiwa na waume zao kwa hoja kwamba wanatimiza sharti la mila hiyo.

Mbakaji kabla ya kuanza kitendo hicho, huwa anaandaliwa chakula maalumu ikiwemo pombe ambayo huwa anakunywa na kuchangamka na hapo ndipo anaaza kubaka.

Kutokana na hali hiyo wanawake wengi walioolewa wilayani Ukerewe ni wabakwaji watarajiwa na wale watakao kataa kubakwa, basi wajiandae kutengwa na ndugu, kunyooshewa vidole na jamii inayowazunguka na mali za marehemu waume zao kutotolewa urithi.

Pia, mjane anayekataa kutakaswa ajiandae kutopata mwanaume wa kumuoa.

Vi kwa z o h i v y o , n d i v y o vinavyowashinikiza wakubali kubakwa na watu maalumu ambao hukodiwa kwa fedha au kulipwa mifungo kwa ajili ya kubaka wajane.

Katika mila hii, mwanamke analazimishwa kufanya tendo la ndoa bila ridhaa yake tena na mtu asiyemfahamu na haandaliwi kwa namna yoyote ile kwa ajili ya tendo hilo.

Wakati kwenye majumba ya utakasaji unafanyikwa kwa njia ya maombi, kwa Ukerewe unafanyika kwa njia ya ubakaji.

Okusomboka ni tendo la ndoa linalohusisha watu wawili, mjane ambaye amefiwa na mume au mke na mwingine ambaye yupo kwa ajili ya kazi hiyo.

Mfano leo hii ikitokea mwanamke akafiwa na mume wake, baada ya mazishi yanafanyika matanga ambapo siku ya nne ya matanga, anakodiwa mtu kutoka miongoni mwa watu wanaokodishwa kwa ajili ya kutakasa mjane na kufanya naye tendo la ndoa tena bila hiari ya mjane.

Ubakaji uliojificha kwenye mila ya Okusomboka (kutakasa) kwa Wakerewe ni tendo ambalo linafanyika kwa maana ya kuhitimisha uhusiano wa ndoa kati ya mume na mke ulioanzishwa kwa tendo la ndoa, hivyo ni lazima uhusiano huo uhitimishwe kwa tendo hilo kutokana na mmoja wa wanandoa kuwa amefariki.

Utakasaji huo unafanyika kwa pande zote yaani mwanake na kwa mwanaume, lakini unatofautiana mazingira unapofanyika.

Mfano, mwanamke anapofiwa na mume wake anakodishwa mtu maalumu wa kufanya naye tendo la ndoa na hapo kunakuwa hakuna maridhiano yoyote kati ya mtakaswaji na mtakasaji, bali maridhiano yanatokana na kile anacholipwa mtakasaji ndipo anafanya tendo hilo.

Lakini, mwanaume anapofiwa na mke wake anaenda mwenyewe mtaani kutafuta mwanamke wa kufanya naye tendo la ndoa wakati mwingine akisindikizwa na wapambe watakaothibitisha kwamba, alipata mwanamke na kufanya naye tendo la ndoa, hivyo anakuwa ametakasika.

Wanafanya hivyo, kwa kuamini kwamba, marehemu wakati anafikwa na mauti hakupata fursa ya mwisho ya kufanya tendo la ndoa hilo na mwenzi wake.

Kwa msingi huo, wanafanya hivyo kama ishara ya kuhitimisha uhusiano wa wanandoa hao, yaani marehemu na yule aliyebaki hai.

Wakerewe wanaamini kuwa, mjane au mgane akishatakaswa ile mikosi yote iliyosababisha kifo cha marehemu inakuwa imeondolewa yote.

Pia wanafanya hivyo kwa kuamini kwamba, marehemu wakati anafikwa na mauti hakupata fursa ya mwisho ya kufanya tendo hilo na mwenzi wake.

Hiyo inakuwa ni ishara ya kumalizika kwa uhusiano wa wanandoa hao, yaani marehemu na yule aliyebaki hai.

UBAKAJI WENYEWE

Mmoja wa wazee anayefahamu mila hiyo ambaye pia aliwahi kufanyiwa mila hiyo, Juma Mtallo (83) mkazi wa Nkilizi katika Kijiji cha Mmakeke wilayani Ukerewe, anasema pindi mwanamke anapofiwa na mumewe, kama kawaida yanafanyika matanga kwa siku kati ya tano na saba kulingana na uwezo wa wafiwa.

Katika kipindi hicho, mjane huyo anatakiwa kuhudumiwa na kuandaliwa chakula na mtu aliyewahi kufiwa na mwenzi wake.

“Anakuwa ndani ya nyumba amefunikwa nguo na wanaoenda kumsalimia na kumhudumia ikiwa ni pamoja na kumpikia chakula ni wale waliowahi kufiwa,” anasema Mtallo.

Anasema, kwa kipindi hicho anakuwa hajaoga. “Siku ya nne ndipo wanaanza taratibu za kumuogesha na akishamaliza ndipo anapelekwa kwa mbakaji (mtakasaji).”

Anaongeza kwamba baada ya mtakasaji kumaliza kazi hiyo, anaondoka kwa majigambo na wakati mwingine akiimba; “Wanaume wafe wanawake wabaki…wanaume wafe wanawake wabaki,” anasema huku akiongeza huwa anaimba hivyo ili wanaume wazidi kufa na yeye azidi kupata kazi ya kubaka wajane.

SIKU YA UBAKAJI

Kwa mujibu wa mila hiyo, siku ya kubaka, mbakaji huwa anaandaliwa chakula kizuri pamoja na vinywaji hasa pombe kwa gharama za familia inayotakaswa.

Mmoja wa wanawake waliowahi kutakaswa, Anna Sebastiane mkazi wa Tarafa ya Ukara Kata ya Bukungu, wilayani Ukerewe anasema, siku mtakasaji anapoenda kutakasa mjane, anapokelewa kwa heshima kubwa.

Anaeleza kwamba wakati mwingine anaweza kumwambia mtakaswaji; “Hebu cheza nione kama unaweza,” anasema yaani aoneshe umahiri wa kutikisa nyonga wakati wa tendo la ndoa.

Anafafanua kwamba, endapo ataona mjane hawezi kutikisa nyonga, anaongeza gharama. Mfano endapo aliwatoza fedha basi atapenda aongezewe kiasi atakachoona kinamfaa au kama ni mifugo kama vile mbuzi, atataka aongezewe mwingine kwa jinsi atakavyoona inafaa.

Hata pale asipovutiwa sura ya mtakaswaji, mtakasaji anapandisha gharama kwa jinsi atakavyoona inafaa.

Anasema, endapo utakasaji utafanyika nyumbani kwa marehemu basi ndani ya nyumba inabidi wawepo watoto wake ambao hawajaolewa.

“Wakati utakasaji unafanyika (ubakaji) watoto wanakuwa wanasikia jinsi Omwezya (mtakasaji) anavyonguruma (akitoa maelekezo kwa sauti nene akimwelekeza mjane jinsi anavyotaka alale au namna ambavyo anataka atingishe nyonga yake) na hapo kitanda kinachokuwa kinatumika ni cha marehemu,” anasema Sebastiane.

Anapoulizwa kama watoto wanasikia hiyo sauti? Sebastiane anacheka kwanza huku akivuta pumzi, kisha anasema;

“Sio watoto peke yake, hata wanaokuwa nje wanafahamu kinachoendelea …si unaona hali ya nyumba zetu (mbovu kiasi kwamba nyingi hazina faragha). Anasema anakuwa anahimiza mtakaswaji atingishe nyonga ili apate raha.

“Watakasaji wengine, hawakuwa na staha na tendo la ndoa, kwani walipokaribia mshindo (kutoa mbegu za uzazi) walipiga kelele kwa kunogewa na uhondo wakati huo huo akiashiria kwamba kazi aliyopewa amehitimisha,” anasema na kuongeza kuwa akishamaliza anavaa nguo na kutoka nje ya nyumba kwa mbwe mbwe kisha kulipwa chake.

Anasema, watakasaji wengine waliondoka wakiimba; “wanaume wafe wanawake wabaki..wanaume wa f e wa n awa k e wa b a k i . ” Anasema hiyo kwa kufurahia kile walicholipwa. “Wakati anaondoka anapigiwa vigelegele na akina mama kwa kufurahia kuhitimisha mila hiyo…mila hii unaweza kuiona ni mbaya, lakini yakishakufika utaona umuhimu wake,” anasema Sebastiane.

Hata hivyo, anasema: “ Mila hii (Okusomboka) ni aibu kwa watoto wanaokuwa ndani ya nyumba wakisikiliza mama yao akitakaswa, huku akihimizwa atingishe nyonga… tendo la ndoa linahitaji faragha, lakini utakasaji hauna faragha na unamdhalilisha mwanamke,” anasema na kuongeza kuwa ni jambo la aibu ndiyo maana tendo la ndoa linahitaji faragha.

Sebastiane anapoulizwa kama mtakasaji anatumia kondomu ili kujikinga na magonjwa, anasema jambo hilo halipo.

Pia anasema, mtakasaji na mtakaswaji wanatakiwa wafanye tendo moja la ndoa (yaani mshindo mmoja) na wasifanye tena tendo hilo maishani mwao, endapo wakirudia watakuwa wamekiuka sharti la mila hiyo hivyo mikosi inaweza kurudia familia ya mjane.

“Kwa hiyo atalazimika atakaswe (abakwe) upya na mtakasaji mwingine, vinginevyo wanaamini kuwa familia yake itaendelea kuandamwa na mikosi,” anasema .

Anataja mikosi hiyo kuwa ni pamoja na familia kuandamwa na vifo na kuugua mara kwa mara.

MASHAHIDI

Mashahidi wanaoshuhudia tukio hilo, wanasema wanakuwepo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tendo hilo limefanyika, ili kuondoa wasiwasi wa wajane kudanganya.

Mjane mwingine, Arodia Gabaseki (64) mkazi wa Kata ya Ulagala, Tarafa ya Masonga wilayani Ukerewe anasema mashuhuda wanakuwa nje katika mazingira ambayo watakuwa na uhakika kuwa tendo hilo linafanyika.

Anasema kwamba, kutokana na wajane kuogopa mikosi, lazima wakubali na kwamba mgurumo wa mtakasaji nao kwa wakati mwingine ni ishara nzuri kwao.

Anaeleza kwamba, mara baada ya kutakaswa anarejea nyumbani akiwa ameinamisha kichwa chini na kupokewa kwa furaha na wanandugu waliopo kwenye matanga, kwa kuwa wanaamini kuwa uhusiano kati ya mjane na marehemu umehitimishwa na hakuna matatizo yoyote yanayoweza kuwapata.

SIFA YA MTAKASAJI

Ofisa wa Taasisi ya Kuboresha Mila na Desturi katika Jamii ya Ukerewe (KUMIDEU), taasisi ambayo inajihusisha kutoa elimu ya kutokomeza mila ya kutakasa wajane, Musiba Kakulu anasema mtakasaji ni mtu anayeonekana hakubaliki ndani ya jamii kutokana na matendo hayo.

Anasema, watakasaji wengi ni walevi, wachafu, wasiokuwa na wanawake na mara nyingi walitegemea kuendesha maisha yao kwa kutegemea malipo wanayopata kwa njia ya utakasaji.

“Kutokana na umuhimu wa mila ya kutakasa, mtakasaji (Omwezya) anakuwa hana umuhimu ndani ya jamii,” anasema Kakulu. Sifa nyingine anasema ni mtu anayejua dawa na anayependa kusimamia mila na desturi.

Pamoja na kuwa na hali hiyo, lakini thamani yao inaonekana pale walipohitajika kutakasa, kwani watu wenye heshima zao ndani ya jamii hawakubali kabisa kutakasa watu ambao tena haijulikani wenzi wao wamefariki kwa magonjwa gani.

“Mtakaswaji kama ni bibi kikongwe, anapata shida kwani mtakasaji anatoza gharama kubwa kama vile ng’ombe wakati uwezo anakuwa hana, lakini ndugu lazima wachangishane ili wampate ng’ombe huyo,” anasema.

Anasema, wakati mwingine mtakasaji anapotakiwa kwenda kwa mtakaswaji na ni mzee sana analazimika atafutiwe usafiri hadi nyumbani kwa mjan
 

5 comments:

  1. Daah ama kweli Uislam umeleta Nuru katika hii Dunia,leo tupo ktk karne ya sayansi na maendeleo lakini baadhi ya watu bado wanaishi ktlk giza mpaka hii leo....daah huu ni msiba mkubwa.kwanza hio sehemu kama kweli ipo basi hapafai hata kuishi,hapo zinaa imeota mizizi kiasi kana kwamba wanaoishi hio sehemu ni wanyama.!kwa kuwa wanyama kwao vyote ni sawa tu.naiomba Serikali iende ikaielemishe hio jamii ubaya wa Zinaa .

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni aibu kubwa sana kuona haya bado yanaendelea katika jamii zetu hapa Tanzania? ukikaa na kufikiri ni kweli uislam umeleta ukombozi hususan kwa mwanamke wa kiafrica

      Delete
    2. Misri kwa waislam walikuwa wanataka ipitishwe sheria ya kuaga marehemu kwa kufanya nae tendo la ndoa (kujamiiana na maiti) sasa sijui unasemaje hapa kuhusu uislam? Ata bongo kuna hii fairwell goodbuy sex watu wanafanya wanasema ni maagizo ya dini ya uislam, clouds fm ktk kipindi cha njiapanda kuna jamaa alitoa ushuhuda kwamaba alishafanya alipofiwa na mkewe akidai aliambiwa ni sheria kwa muislam kuitekeleza. LAKINI kuna ustadhi alihojiwa akasema sio mafundisho ya uislam ni mila potofu tu. Hivyo hapa usiweke mambo ya dini flani wewe laani tu hizi mila potovu. Na kama una kumbukumbu ktk hii habari kuna mtu mwenye jina la kiislam soma hapa "Mmoja wa wazee anayefahamu mila hiyo ambaye pia aliwahi kufanyiwa mila hiyo, Juma Mtallo (83) mkazi wa Nkilizi katika Kijiji cha Mmakeke wilayani Ukerewe....."

      Delete
    3. Uislam umeleta Nuru gani hiyo unasema? Nuru ama giza? Uislamu bado unawakandamiza wanawake, kwa mfano nchini Saudi Arabia wanawake hawaruhusiwi kuendesha magani na tukienda mbali zaidi hata kuna baadhi ya nchi wanawake wa kiislamu hawaruhusiwi kwenda shule kusoma. Wao badala ya kujenga shule na vyuo fedha wanafadhili ugaidi. Hiyo ndo nuru unasema? Waislamu hawawezi kupambana kwa hoja na istoshe ndio wamiliki wakubwa wa majini ambayo ndiyo yanauwa watu na kusababisha ajali nyingi. Sasa unaposema Nuru sijui iko wapi hiyo? Kuna baadhi ya misikiti mi naijua imegeuzwa kuwa ndo makutano ya wachawi na kupangia kufanya uchawi kuloga watu halafu wanakazana sana kuswali, hiyo ndo Nuru? Usiingize swala la dini hapa vinginevyo tutakushambulia na utakosa hoja za kujibu. Sisi tunaushaidi wa kitaalam.

      Delete
  2. Hapa issue ya uislam inakujaje jamani, mimi nadhan jambo kubwa hapa ni kuhakikisha jamii kama hii inapata elimu juu ya uprimitive walionao ili waweze kuacha, viongozi washirikishe taasisi na asasi mbalimbali kama vile madhehebu mbalimbali ya dini na misikiti, wanaharakati wa jinsia, lakini hasa mashuleni ambapo ndio watoto bado wanachipukia hivyo wanapandikizwa mbegu njema na wao watakuwa mabalozi wazuri kwa wazazi wao

    ReplyDelete