23 August 2013

REA YAJIDHATITI KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI Na Steven William, Muheza
IMEELEZWA kwamba hadi ifikapo mwaka 2015 huduma ya nishati ya umeme itakuwa imesambazwa vijijini kwa asilimia 30 nchi nzima kutoka asilimia 21ambayo ipo hivi sasa.Hayo yalisemwa na Mtaalam mshauri na mkufunzi, Mzumbe Mu s a k u t o k a Wa k a l a wa kusambaza nishati vijijini ( REA) katika mafunzo ya kuhudumia na kurekebisha mifumo ya umeme wa jua ambayo yamefanyika wilayani Muheza.

Alisema kuwa wakati mpango huo wa usambazaji huduma ya nishati inaanza kupitia REA umeme ulikuwa umesambazwa asilimia 10 nchini lakini baada ya mradi huo kuanza imefikia asilimi 21 sasa kutoka asilimia 10.Musa alisema kuwa mwanzo wa usambazaji umeme vijijini ilikuwa asilimia mbili kitu ambacho tofauti na sasa asilimia 21 toka REA waingie kusambaza nishati hiyo vijijini.
Musa alisema kuwa baada ya kutoa mafunzo hayo ya ufungaji vifaa vya umeme jua kwa vijana 35 watakwenda kufanya kazi kwa vitendo kwa kufunga katika Zahanati tatu wilayani Muheza.Al i t o a c h a n g amo t o kwa halmashauri ya Wilaya ya Muheza pindi nishati hiyo itakapofungwa watenge bajeti ya kufanya matengenezo kama vile taa zikiungua na kununua betri.
Hata hivyo Ofisa Maendeleo ya Jamii wilayani Muheza, Vije Mfaume alimhakikishia mkufunzi huyo kuwa watatenga fedha za kuendelea kuzihudumia sola hizo pindi zikiharibika.Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Amiri Kiroboto alishukuru huduma hiyo kufika wilayani humo.
Kwa upande wake mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Muheza, Paul Moshi ambae alimwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Subira Mgalu akifungua mafunzo hayo ya siku nane alisema kuwa mafunzo hayo yatafanikisha kupata umeme katika vijiji vya Muheza.Alisema kuwa ifikapo mwaka 2015 wanataka kuona wilaya ya Muheza vijiji vyote vinakuwa na nishati ili kuendeleza huduma za jamii na kuwahamasisha wananchi vijijini kutumia nishati hiyo

No comments:

Post a Comment