23 August 2013

CCM KUTOA MIKOPO KWA WANACHAMA HAINa Heri Shaaban
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinatarajia kuanza kuwakopesha mikopo ya riba nafuu wanachama wake walio hai ili kuwawezesha kuwa na maendeleo na kukuza mitaji yao ya biashara.Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa CCM, JeremiahWambura wakati wa mkutano wa wanachama wa CCM katika Mtaa wa Kifuru Kata Kinyerezi
. Wambura alisema mikakati hiyo ya kutoa mikopo inatarajia kuanza hivi karibuni ambapo CCM inafanya mazungumzo na wafadhili mbalimbali watakaosimamia utoaji wa mikopo hiyo.
Alisema kuwa masharti ya kujiunga katika mikopo hiyo ni lazima awe mwanachama na mwenye kadi ya CCM ambapo ada ya kujiunga ni sh.20,000 ambapo mpango huu unatarajia kusambaa nchi nzima."Mikopo hii tunatoa kwa wanachama wetu waweze kujishughulisha katika biashara na kukuza mitaji yao na kuondokana na umaskini," alisema Wambura.
Alisema CCM imethubutu na inaweza na kwa sasa inasonga mbele na ambapo katika Afrika ni nchi ya pili kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hivyo juhudi zaidi zinaendelea ili kuwawezesha Watanzania kuwa na maendeleo

No comments:

Post a Comment