23 August 2013

MIUNDOMBINU YA MAJI YAHUJUMIWA



. Na Severin Blasio, Morogoro
WATU wasiofahamika wame h u j umu kwa kung'oa na kupasua mabomba ya maji katika kijiji cha Pangawe kilichopo Kata ya Mkambarani wilayani Morogoro.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa watumiaji maji wa Mkambarani, Ruben Chabaliko hujuma hiyo inadaiwa kuanza Julai 15 zimeharibu bomba kuu lenye ukubwa wa inchi 22 zinadaiwa kusababishwa wananchi ambao hawaungi mkono huduma hiyo ya maji kugharimiwa kama ilivyopendekezwa na Jumuia ya watumiaji maji katika Kijiji cha Mkambarani
"Hujuma hizo zilianza tangu Julai 15 kwa kulipasua bomba kuu lenye ukubwa wa nchi 22 linalotoka milima ya Uluguru katika maeneo ya mlima Ng'alo-Kiloka na baadae kurudiwa tena Julai 17 katika eneo la mashamba ya mkonge Pangawe lakini hali hiyo ikarudia tena Agosti 20 maeneo ya Mkongeni kwenda Mkambarani"alifafanua Chabaliko.
Akitoa ufafanuzi wake kwa waandishi wa habari, Chabaliko alisema wananchi wanasikitishwa na Serikali kushindwa kutoa ushirikiano katika kulikabili suala hilo.Kutokana na hujuma hiyo Chabaliko alisema wananchi sasa wanapata usumbufu wa maji na kufanya baadhi ya taasisi na makampuni ikiwemo Gereza la Mtego wa Simba na Kiwanda cha Tumbaku cha Alliance One na Zahanati kukosa huduma hiyo.
Hata hivyo tayari uharibifu huo umeigharimu ofisi ya watumia maji katika Kijiji cha Mkambarani kupata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya matengenezo ili kunusuru wakazi wasipate adha ya kukosa maji.Alipotafutwa kujibu madai ya kuwapuuza wananchi juu ya tukio hilo Mkuu wa wilaya hiyo, Said Amanzi alisema yeye hahusiki na matatizo hayo huku akiwataka waandishi kuonana na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Julius Madiga na viongozi wa Serikali za vijiji

No comments:

Post a Comment