Na Fatuma Rashid
SHIRIKISHO la Kimataifa la Ngumi za
Kulipwa (WBF), limeshukuru Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania TPBO kwa
kufanikisha pambano la ngumi la kimataifa uzito wa kati.Akizungumza na waandishi wa habari Dar
es Salaam jana wakati wa kumtambulisha bondia Phil Wiliums kutoka marekani Rais
wa WBF, Howard Goldberg alisema pambano hilo litasaidia kukuza mchezo wa ngumi
hapa nchini
.Goldberg alisema katika mpambano huo
kati ya Francis Cheka na Wiliums, mshindi atakwenda kupambana nchini Ujerumani
Oktoba, mwaka huu na mbali na mpambano huo pia nchi ya Colombia imeomba pambano
na Cheka.Alisema wameamua kuwapambanisha bondia,
Thomas Mashali na Mada Maugo wote kutoka Tanzania ambao watawania ubingwa wa
Dunia uzito wa kati, ili kuendeleza vipaji vya ngumi kwa mabondia ambao bado
umri wao unaruhusu kuendelea na fani hiyo.
"Francis Cheka hivi sasa umri wake
umeshakuwa mkubwa, hivyo tumeona ni bora kuzidi kukuza vipaji vya mabondia hawa
wenye umri ambao bado ni mdogo, ili kukuza vipaji vyao na hapo baadaye wazidi
kufanya vizuri," alisema.Naye bondia Wiliums, alisema amekuja
kwa ajili ya kazi moja na atahakikisha anachukua mkanda huo, kwani anajiamini
kuwa yeye ni bondia aneyefanya vizuri katika mchezo huo.
Kwa upande wake, Botha 'White Buffalo'
alisema katika mpambano huo anatarajia kuona kitu cha pekee kutoka kwa mabondia
hao, ili waweze kupata nafasi za kushiriki mapambano mengi zaidi."Mabondia hawa ninauhakika ni
wazuri naamini wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mpambano, hivyo kama wakifanya
vizuri ninauhakika wataweza kushiriki mapambano mengi zaidi,"alisema.Naye
mratibu wa pambano hilo, Jay Msangi alisema mpambano huo wa kimataifa ni wa
kwanza kufanyika hapa nchini, hivyo itasaidia kuutangaza vizuri mchezo wa ngumi
ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment