Na Amina Athumani
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira
amesema Rais Jakaya Kikwete amesisitiza atawajibisha mawaziri wote
watakaozembea kutimiza majukumu yao ikiwemo mipango ya maendeleo nchini.
Hayo aliyasema juzi jijini Dar es Salaam wakati akieleza mkakati wa
Serikali katika kutekeleza mfumo ujulikanao kama 'Matokeo Makubwa Sasa'. Waziri Wassira alisema, katika utekelezaji wa mfumo huo watendaji hasa
mawaziri watakaozembea majukumu yao watawajibishwa na kiongozi mkuu wa Serikali
ambaye ni Rais.
Alisema, lengo la mfumo huo ni kuleta matokeo mazuri ya uchumi kwa muda
mfupi. Pia alisema, mfumo huo utagharimu zaidi ya sh. trilioni 8.9 kila mwaka
kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo Serikali itawekeza kiasi cha sh. trilioni
2.9 huku sekta binafsi zikitarajiwa kuwekeza sh. trilioni 6.
Alisisitiza kuwa, mafanikio ya mfumo huo yatategemea na ushiriki mkubwa
kutoka katika sekta binafsi
Wa z i r i Wa s s i r a alizihakikishia sekta binafsi kwamba Serikali
iko pamoja nao katika shughuli za kibiashara.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi na Makampuni
Binafsi nchini, Ally Mafuruki alipongeza hatua ya Serikali kusitisha kuagiza
samani nje ya nchi kwa ajili ya matumizi ya Serikali ambayo sasa itazinunua
katika soko la ndani. Mwenyekiti huyo pia ameitaka Serikali iweke v i g e z o v y a u b o r a
i l i wazalishaji wa ndani wa samani hizo wazitimize.
No comments:
Post a Comment