Na Elizabeth Mayemba
MWENYEKITI wa klabu ya Simba Aden Rage
ameamuru timu hiyo irudi Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki
na Mafunzo ya Zanzibar itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa lengo
la kuwatambulisha wachezaji wao kutoka Burundi
.Wachezaji hao ni Amisi Tambwe, Gilbert
Kaze na kiungo wao za zamani Henry Joseph aliyetokea katika klabu ya
Kongsvinger ya Norway.Beki Kaze na mshambuliaji Tambwe awali
walishindwa kutambulishwa baada ya kushindwa kupatia Hati zao za Uhamisho
(ITC), ambapo kwa sasa tayari wamepatiwa.
Awali Kocha Mkuu wa timu hiyo Abdallah
Kibadeni alikataa timu kucheza mechi hiyo kwa madai icheze Moshi mkoani
Kilimanjaro baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania na JKT Oljoro,
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, ambao Simba ilishinda 1-0.
Hata hivyo baada ya viongozi wa juu
kukaa wakakubaliana timu yao icheze na Mafunzo ya Zanzibar badala ya Machava FC
ya Moshi.Rage alilazimika kwenda Burundi kufuata
ITC za wachezaji hao mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuona zinachelewa
kufika nchini, hivyo kuwachelewesha pia kuanza kazi.
Wachezaji wengine wa kigeni wa Simba,
Waganda Joseph Owino na Abel Dhaira, wamecheza mechi zote mbili za awali za
Ligi Kuu, kutokana na kukamilishiwa taratibu zote za uhamisho na kuwa na vibali
vya kufanya kazi nchini.
K a z e n a T a m b w e waliosajiliwa kutoka mabingwa wapya wa Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati,Kombe la Kagame, Vital'O ya wakati wa ufunguzi
wa Ligi Kuu walikuwapo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora kuishuhudia timu
yao ikilazimishwa sare ya 2-2 na Rhino Rangers.
No comments:
Post a Comment