Na Fatuma Rashid
MABONDIA Phil Wiliums wa Marekani na
Francis Cheka, wamepima uzito kwa ajili ya pambano lao la ngumi la ubingwa wa
WBF la uzito wa kati linalotarajiwa kufanyika leo, kwenye Ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kupima uzito huo, Rais wa
Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) ambao ni wasimamizi wa ndani
wa mpambano huo, Yassin Abdallah 'Ustaadhi' alisema pambano hilo litautafanya
mchezo wa ngumi kuzidi kusonga mbele nchini.
Ustaadhi alisema katika sheria za
Shirikisho la Kimataifa la Ngumi za Kulipwa (WBF), bondia anatakiwa kutetea
mkanda huo ndani ya miezi tisa."Bondia atakayenyakua mkanda huu
atatakiwa kuutetea kwa muda wa miezi tisa na hatoruhusiwa kushiriki mpambano
wowote hadi pale atakapoomba na kuruhusiwa na WBF," alisema.
Alisema pambano lingine kati ya Alphonce Mchumiatumbo na Deandre Mccole
kutoka Marekani katika uzito wa juu usio wa ubingwa, halitachezwa kutokana na
bondia huyo wa Marekani kuchelewa kuwasili nchini.
No comments:
Post a Comment