- POLISI WARUKA:WAISLAMU TUNATAKA UCHUNGUZI
- MADAKTARI MOI WAWEKA MAMBO HADHARANI
Na
Waandishi Wetu
TUKIO la Katibu wa Jumuiya ya Waislamu
Tanzania, Shekhe Ponda Issa Ponda, kupigwa risasi limetawaliwa na siri nzito,
kuanzia tukio lilipotokea, jinsi alivyosafirishwa kutoka Morogoro hadi jijini
Dar es Salaam na baadaye kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Uzito
wa usiri wa tukio hilo
unatokana na kutojulikana moja kwa moja kwa mtu aliyehusika kumpiga Shekhe
Ponda risasi, hali inayoibua maswali mengi kuliko majibu
Tukio
la Shekhe Ponda, la kupigwa risasi bega la kulia na kuvunja mfupa mkubwa wa bega
hilo
limethibitishwa na Madaktari wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) waliomfanyia
uchunguzi kupitia Ofisa Ustawi Mwandamizi wa taasisi hiyo, Mary Ochieng.
Hata
hivyo, taarifa za Shekhe Ponda kupigwa risasi zimekanushwa vikali na Makao
Makuu ya Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile, ambako tukio lilitokea.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ochieng, alisema Shekhe Ponda
alipokelewa hospitalini hapo saa 5 asubuhi na baada ya vipimo vya madaktari imegundulika
amevunjika mfupa mkubwa wa bega la kulia, ambapo risasi imeingilia mbele na
kutokea nyuma.
Alisema
hali yake ilikuwa inaendelea vizuri na alitarajiwa kufanyiwa upasuaji jana.
Akizungumzia
hali hiyo mpwa wa shekhe Ponda Bw. Isiaka Rashid, baada ya kupata taarifa hizo
walianza kufuatilia na kuamua kwenda mkoani Morogoro lakini kabla ya kufika
huko waliambiwa amepelekwa Dar es Salaam. Alisema walikutana naye maeneo ya
Magomeni akiwa kwenye teksi.
Alisema
walimpeleka Muhimbili ambapo walitakiwa kuwa na PF3 hivyo walienda Kituo cha Polisi Salender
Bridge na kupewa PF3
kisha kuendelea na taratibu zingine.
Ha
b a r i z i n a e l e z a k uwa makachero wa polisi walipiga kambi Muhimbili
tangu saa 11 asubuhi jana waliendelea kumsubiri hadi alipofikishwa saa 5.
Aliingizwa katika chumba cha wagonjwa wa dharura saa saba mchana, huku
makachero wakiwa wamejaa eneo la Muhimbili.
Habari
kutoka ndani ya Polisi zilieleza kuwa Shekhe Ponda, alikuwa chini ya ulinzi,
lakini isingekuwa rahisi kumfunga pingu kutokana na hali yake.
Magari
ya Polisi ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) yalikuwa yameegeshwa ndani ya
uzio wa Kikosi cha Zima Moto eneo la Faya, yakiwa na askari waliojidhatiti kwa
silaha.
TAMKO LA POLISI MAKAO MAKUU
Jeshi
la Polisi Makao Makuu limewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki
wakati suala hilo
la Shekhe Ponda, likishughulikiwa kisheria.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, ilieleza kuwa,
kufuatia tukio hilo, timu inayoshirikisha
wajumbe kutoka Jukwaa la Haki Jinai ikiongozwa na Kamishna wa Jeshi la Polisi,
Issaya Mngulu, imeanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Taarifa
hiyo ilieleza mazingira ya tukio hilo,
kuwa juzi mchana maeneo ya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya
Morogoro, kulifanyika kongamano la Baraza la Idi lililoandaliwa na Umoja wa
Wahadhiri wa mkoani humo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, dakika 10 kabla ya kongamano hilo kumalizika, alifika Shekhe Ponda, ambapo
alizungumza kwa muda mfupi.
Taarifa
hiyo ilieleza kuwa kongamano hilo
lilifungwa saa 12:05, ambapo walianza kutawanyika huku baadhi ya watu wakiwa
wamezingira gari dogo alilokuwa amepanda, Shekhe Ponda.
“Baada ya kutoka katika eneo hilo, Polisi
walizuia gari hilo
kwa mbele kwa nia ya kutaka kumkamata kutokana na kutuhumiwa kwa kosa la kutoa
maneno ya uchochez
sehemu mbalimbali nchini yenye lengo la kusababisha
uvunjifu wa amani,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza;
“Askari baada ya kutaka kumkamata, wafuasi wake
walizuia asikamatwe kwa kuwarushia mawe askari.” Kufuatia purukushani hizo,
askari walipiga risasi hewani kama onyo la
kuwatawanya.
Taarifa hiyo ya Polisi inaeleza kuwa wakati wa
vurugu hizo, wafuasi wa Shekhe Ponda walifanikiwa kumtorosha Shekhe Ponda.
“Hivi sasa imethibitika Shekhe Ponda yuko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
akitibiwa jeraha katika bega la mkono wa kulia linalodaiwa alilipata katika
purukushani hizo,” ilieleza sehemu ya taarifa hizo.
POLISI MOROGORO
Kwa upande wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro,
limesema kuwa halijapokea taarifa yoyote ya kupigwa risasi kwa Shekhe Ponda
wakati wa mhadhara uliofanyika jana kama
ilivyovumishwa katika maeneo mengi nchini.
Jeshi hilo, limesema
linamsaka kwa udi na uvumba mara baada ya kupewa kibali cha kumkamata kutoka
Makao Makuu ya Jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema kuwa ofisi yake
haijapokea taarifa ya kupigwa risasi kwa mtu yeyote aliyekuwa katika mhadhara
huo, zaidi ya kijana mmoja aliyesadikiwa kupigwa tofali kichwani katika
mhadhara huo ambaye alifika Polisi kupatiwa PF3.
Hata hivyo, kamanda huyo alisema kuwa jeshi lake linaendelea
kumsaka, Shekhe Ponda na wafuasi wake kwa kosa la kufanya vurugu na kusababisha
hasara katika Hospitali ya Mkoa Morogoro, ikiwa pamoja na kuwazuia askari
kufanya kazi yao.
Alisema kuwa hadi sasa kumekuwa na uzushi na utata
juu ya jambo hilo katika maeneo mengi ya kuwa
Shekhe Ponda, amepigwa risasi na Polisi, hali ambayo mpaka sasa hakuna ukweli
juu ya jambo hilo,
kwa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha.
PROF. LIPUMBA AFUNGUKA
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa.
Ibrahim Lipumba, amelaani kitendo cha Shekhe Ponda, kupigwa risasi, huku
akilituhumu Jeshi la Polisi kuwa limehusika.
Kufuatia tukio hilo, Prof. Lipumnba ameitaka Serikali
kuhakikisha Shekhe Ponda anapata matibabu haraka na kufanya uchunguzi na
kumfikisha kwenye vyombo vya sheria askari aliyefanya unyama huo.
Pia alielekeza lawama zake kwa Polisi, akidai kuwa
lilikuwa kikwazo wakati wa kutoa PF3 ili Shekhe Ponda aweze kupata matibabu.
Alidai kuwa askari waliofanya unyama huo mkoani Morogoro akamatwe mara moja na
achukuliwe hatua za kutesa raia.
KAULI YA PINDA YA
PIGA TU
Prof. Lipumba alisema kupigwa risasi kwa Shekhe
Ponda, kunatokana na kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakati wa
Bunge lililopita kuwa watakaokaidi kutii sheria lazima wapigwe tu.
Alisema kuwa vyombo vya dola vinahatarisha amani,
hivyo alimtaka Rais Kikwete kuchukua hatua ili kunusuru nchi isiingie kwenye
machafuko ya kidini.
MSIMAMO WA CHADEMA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimelaani
tukio hilo na
kimesema kuwa hali hiyo ni matokeo ya kauli ya Waziri Mkuu, Pinda. Mkurugenzi
wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alisema; “Kupigwa risasi kwa Ponda
ni matokeo ya kauli ya Pinda ya kuwataka polisi wapige raia wanaokaidi.”
Mnyika alisema atapeleka hoja Bungeni ya kutokuwa
na imani na Waziri Pinda kutokana na matukio yanayotokea.
MSIMAMO WA WAISLAMU
Wakati huo huo, wafuasi wa Shekhe Ponda, wametoa
tamko la kuitaka Serikali imchukulie hatua Polisi anayedaiwa kumpiga risasi na
kuueleza umma mazingira ya tukio hilo.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana katika Msikiti wa Mtambani
na Amiri Mkuu wa Baraza Kuuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe
Yusuph Kundecha, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema wanaamini kwamba hatari ya wailsamu ipo
mikononi mwa vyombo vya dola. Alisema kuanzia sasa Waislamu hawana imani tena
na polisi.
Alisisitiza kuwa; “Tunataka uchunguzi wa wazi
ufanyike, hatua zichukuliwe kwa askari aliyefyatua risasi na hatua hizo
ziwaridhishe waislamu kinyume cha hapo watatafakari upya nini wafanye,”alisema.
Alisema kumpiga risasi ni hatua inayolenga
kuwafunga mdomo waislamu pasipokujua kwamba kufanya hivyo hakuwezi kuwaziba
midomo. Alisema kuwa Shekhe Ponda alikuwa anaeleza malalamiko ya waislamu na
hakuwa anafanya uchochezi kama inavyodaiwa na
vyombo vya dola.
Alisema matatizo ya waislamu ambayo alikuwa
anaeleza siyo siri na Serikali inayafahamu muda mrefu. Alisema kuwa serikali
ilikuwa na uwezo wa kumkamata Shekhe Ponda na kwenda kupata maelezo ya kutosha
tofauti na ilivyofanyika.
Naye Wakili wa Shekhe Ponda, Juma Nassor, aliitaka
serikali kutolipuuza jambo hilo
vinginevyo nchi itaingia kwenye matatizo. Alisema kitendo walichofanyiwa Shekhe
Ponda ni ujumbe mbaya kwa waislamu.
Imeandikwa na Goodluck Hongo, Gladness
Theonest, Ramadhan Libenanga, Rachel Balama na Anneth Kagenda.
serikali ya kikwete ni ya kikumaaa,mana wanatakata waislam tuanzishe mtiti na litakuja vagii si la kitoto mda c mrefu
ReplyDeleteYANAYOTOKEA MISRI HAYANA MUDA YATATOKEA TANZANIA INAPOFIKIA KIONGOZI WA SIASA ANAONEKANA WAZIWAZI AKITETEA UDINI INASHANGAZA HATA WALE WANAOITWA MAKAFIRI WAMEJISAHAU KUWA DAMU YAO ITATUMIKA KUINYWESHA TANZANIA IKUMBUKWE IWAPO KAFIRI ATAUAWA HAKUNA MSIBA,MATANGA AU KUMUUA ALIYEUA KAFIRI NCHI YA MISRI CHINI YA ABDUL NASSAR HAKUKUWA NA HUU UDINI AMBAO UMEIGAWANYA MISRI KATIKA MAPANDE MAWILI KITAKAFUATA NI VITA VYA JIHAD TUONE WANAOTUMIA UPANGA NA WANAPIGA SERA YA JICHO KWA JICHO NA JINO KWA JINO HAIPO HIVI SIJUI WANA UPAKO WA MUNGU KUWAPIGANIA KAMA SIO KUANGAMIZWA WOTE KAMA WAFIA DINI WA UGANDA KIONGOZI WA DINI ANATHUBUTU KUJINADI KUWA JINI YAKE NDIO ITAMPELEKA IKULU AMEJIDANGANYA NI VEMA AACHE MARA MOJA NI BORA AINGIE KWENYE NYUMBA YA IBADA AKASALISHE ASITUZENGUE ILA ONYO KWA WANAOITWA MAKAFIRI MUTAJIFUTA KWENYE USA WA DUNIA IKIZINGATIWA LENGO LA "NEW WORLD ORDER" NI KUPUNGUZA IDADI YA WATU DUNIANI IBAKIE BILIONI MOJA TU
ReplyDeleteProfessor Lipumba tunajua wewe ni mfuasi wa Sheikh Ponda kwani hata alipoachiwa huru/kupewa kifungo cha nje wewe ulijumuika na wafuasi wa Ponda kwenda kumpa pole na ukanukuliwa na vyombo vya habari ukiunga mkono hoja za ponda. Kumbuka unautafuta urais 2015, labda usigombee, lakini kama utagombea basi nakushauri uachanae na mawazo hayo hutapata kitu. Umeonyesha kuegemea upande mmoja wa dini. Matukio ya kumwagiwa tindikali viongozi wa bakwata Arusha na mashehe na wageni huko Zanzibar hujajitokeza kulaani kwa nguvu namna hii. Hatutaki nchi hii isitawalikie na kupoteza misingi ya amani na dini zisitumike kuchochea uvunjifu wa amani. Vurugu zikaiza hazichagui dini, kabila wala utaifa. Angalia kinachotokea, Iraq, Syria, Afghanistan, Pakstan na kwingineko, yote hiyo nikutokana na kulipiza kisasi baina ya kundi moja na jingine kwa dhana ya kuonewa. MWENYE MACHO HAMBIWI TAZAMA.
ReplyDeleteKIJANA ACHA KUTUMIA MIGUU AU TUMBO KUFIKIRI! HEBU ACHA CHUKI TUMIA MAKILI ULIYOTUNUKIWA NA M/MUNGU! REGARDS
Deleteserikali ya Tanzania haina dini kutegemea kuwarubuni waumini wa dini yako tu kukupigia kura kwenda ikulu ni kujidanganya mtu wa aina hiyo amefilisika kisiasa labda upanga utumike kumwingiza madarakani na wala si vinginevyo kutegemea kutawala makafiri kwa upanga hizo ni enzi za ANALOJIA SI RAHISI
ReplyDeleteMMEISHAAMBIWA KANISANI KUWA LIPUMBA NI MDINI! ILA MASLAHI YA WAISLAMU YANAPOPIGANIWA NDIPO UDINI UNAJITOKEZA VICE VERSA IS TRUE! MWAMBIENI NA BABU YENU BR,SLAA!REGARDA!!
DeleteSheikh Ponda ni mtanzania kama watanzania wengine. Sheikh Ponda ni mkosaji kama wakosaji wengine kama ilivyo zamani Mh. Mrema au Mchngaji Mtikila ambaye alikuwa kila kukicha alikuwa anaitukana serikali na viongozi wake. Mchungaji mtikila amewahi kustakiwa mara nyingi sana kwa kauli zake. Sheikh Ponda kama Mtikila hawako tofauti. Cha ajabu Sheikh Ponda anaonekana kama mtu si wa kawaida hadi kuipelekea Serikali kutumia fedha za walipa kodi kwa kumpeleka mahakamani kwa magani sita sita na hata helikopta. Serikali na hasa vyombo vya dola mnamkuza bure Sheikh Ponda. Kwake na kwa waumini wake anaonekana kama "HERO" shujaa. Gharama hizo mnazotumia kumlinda Ponda zitumike katika kununua hata PANADOL ambazo zimeadimika sana katika hospitali za serikali.
ReplyDelete