20 August 2013

PONDA ASOMEWA MASHITAKA MOROGORO



Ramadhani Libenanga na Rehema Mohamed
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda, j a n a ame p a n d i s h w a kizimbati katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Morogoro, chini ya ulinzi mkali wa askari polisi baadhi yao wakiwa na mbwa.

Jeshi la Polisi lilitumia helikopta yao kumsafirisha Shekhe Ponda hadi katika Uwanja wa Ndege wa Gofu, mkoani humo. Katika kesi hiyo, Shekhe Ponda alisomewa mashtaka matatu na wakili wa Serikali, Bw. Bernard Kongola mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Bw. Richard Kabate.
Bw. Kongola alidai Agosti 10 mwaka huu, katika eneo la Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, Shekhe Ponda aliwaambia Waislamu kuwa; “Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti.
“Kamati hizo zimeundwa na Baraza Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA), ambao ni vibaraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Serikali.
“Kama watajitokeza kwenu watu na kujitambulisha kama wao kamati za ulinzi na usalama za misikiti, fungeni milango na madirisha ya msikiti muwapige,” alifafanua Bw. Kongola.
Aliongeza kuwa, kauli hiyo iliumiza imani za watu wengine jambo ambalo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa, Mei 9 mwaka huu.
Alisema Hakimu Nongwa alimtaka Shekhe Ponda kuhubiri amani ndani ya mwaka mmoja hivyo kauli aliyoisema ni kinyume na kifungu cha Sheria namba 124 cha mwaka 2002.
Shekhe Ponda alilikana shtaka hilo ambapo Bw. Kongola alisema, katika shtaka la pili Agosti 10 mwaka huu, katika eneo la Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, mkoani humo, aliwaambia Waislamu Serikali ilipeleka jeshi Mtwara kuzuia vurugu zilizotokana na gesi.
Alidai Shekhe Ponda katika vurugu hizo jeshi lilifanya mauaji, kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa Mkoa huo ni Waislamu, lakini Serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji na kudai ni mali yao.
Aliongeza kuwa, Shekhe Ponda alidai asilimia 90 ya wakazi wa Loliondo ni Wakristo, Bw. Kongola alisema maneno hayo yaliumiza imani za watu wengine jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha sheria 129 cha mwaka 2002, shitaka ambalo lilikataliwa na mshtakiwa Shekhe Ponda.
Katika shtaka la tatu ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Agosti 10 mwaka huu, eneo la Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, mshtakiwa huyo alidaiwa kuwalisha maneno ya uwongo Waislamu juu ya sakata la Mtwara, Loliondo.
Alisema kauli hiyo ni kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002, shtaka ambalo Shekhe Ponda alikana.
S h e k h e P o n d a a l i k uwa akitetetewa na wakili Ignas Pungu na Bantalomeo Tarimo wakati upande wa Serikali alikuwepo Bw. Kongola, Gloria Rwakibalila na Asnab Mhando.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Bw. Kongola aliiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi umekamilika hivyo iliahirishwa hadi Septemba 2 mwaka huu.
Upande wa utetezi uliomba kesi hiyo isikilizwe Agosti 26 mwaka huu ambapo Hakimu Kabate alilazimika kuahirisha kesi kwa muda na baada ya kurudi, aliipanga Agosti 28 mwaka huu, kwa ajili ya kusikilizwa.
Mawakili wa utetezi walisema, sababu za kuomba isikilizwe mapema ni ugonjwa wa mteja wao hivyo anahitaji kupatiwa matibabu ya mara kwa mara na uangalizi wa karibu.
Ulinzi uliimarishwa katika eneo la mahakama ambapo msafara wake wakati akipelekwa mahakamani ulikuwa na magari matatu ya Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Shekhe Ponda alirudishwa Uwanja wa Ndege wa Gofu saa sita mchana na kupanda helikopta ya polisi iliyomrudisha
hadi Dar es Salaam na kupelekwa mahabusu ya Segerea.
Ponda afutiwa mashtaka
Ka t i k a h a t u a n y i n g i n e , Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), amemfutia Shekhe Ponda mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
DPP aliwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea na kesi dhidi ya mshtakiwa huyo mahakamani hapo jana.
Mshakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na kesi hiyo mbele ya Hakimu Helleni Liwa wa mahakama hiyo ambapo jana asubuhi Shekhe Ponda alifikishwa mahakamani hapo.
Mbele ya Hakimu Liwa, wakili wa Serikali Tumaini Kweka aliieleza mahakama hiyo kuwa, DPP amewasilisha mahakamani hapo hati ya kutoendelea na mashtaka dhidi ya mshtakiwa hivyo anaomba kumfutia mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Hakimu Liwa alikubaliana na ombi hilo na kumfutia mashtaka mshtakiwa ambaye aliondolewa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Shekhe Ponda alisomewa mashtaka ya uchochezi Agosti 14 mwaka huu akiwa kitandani katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), akiwa chini ya ulinzi wa polisi tangu Agosti 9 mwaka huu, alipofikishwa hospitalini hapo kwa matibabu akitokea mkoani Morogoro.
Kiongozi huyo alifikishwa hospitalini hapo baada ya kudaiwa kupigwa risasi ambayo hata hivyo, si MOI wala polisi waliothibitisha.
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam, ililazimika kuhamia hospitalini hapo kutokana na kulizwa Shekhe Ponda ambapo Bw, Kweka, alimsomea mashtaka hospitalini hapo na kudai kuwa, Shekhe Ponda anatuhumiwa kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini alikana kutenda kosa hilo.

1 comment:

  1. Majeraha na Majeruhi ya UKWELI ni anayajua asemaye na kuandika Urongo. Kama hvo Umezungumzwa Ukweli Ubeba wa UMETUMIKA,HVO mto hauvukwi.

    ReplyDelete