20 August 2013

LAAC YASHTUKIA UBADHIRIFU ILALAKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeunda kamati maalumu ya kufanya ukaguzi wa hesabu za Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam kwa madai ya kuwepo ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka, anaripoti Grace Ndossa na Anneth Kagenda

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Rajabu Mbarouk, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.Alisema hivi sasa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh (CAG), anakagua hesabu hizo kwa umakini zaidi ili kubaini ubadhirifu uliopo.
“Ni mwezi wa pili sasa CAG anakagua mahesabu ya manispaa hii, pia kuna matumizi mabaya ya madaraka, kuna utata ambao umejitokeza kwa baadhi ya madiwani wa manispaa hii, wanamtaka Mkurugenzi aliyesimamishwa kazi Bw. Gabraeli Fuime.
“Madiwani wengine wanamtaka Mkurugenzi aliyepo sasa hivyo tunashindwa kuelewa mvutano huu wa nini,” alisema.Aliongeza kuwa, baadhi y a wami l i k i wa ma b a n g o wameilalamikia manispaa hiyo kwa kuwanyanganya na kuwapa kampuni nyingine hali ambayo imeleta utata.
Bw. Mbarouk alisema manispaa hiyo imekuwa ikilalamikiwa sana na wananchi pamoja na wabunge hivyo CAG akikamilisha ukaguzi huo, taarifa itatolewa.Hata hivyo, alisema mvutano uliopo kwa madiwani hao unaonekana kuna masilahi binafsi kati yao na Mkurugenzi aliyesimamishwa kazi.

No comments:

Post a Comment