ONGEZEKO la usafiri wa pikipiki nchini
kwa asilimia kubwa, umeondoa usumbufu kwa wasafiri wenye kipato cha chini wasio
na uwezo wa kukodi taksi.Kutokana na msongamano wa magari nchini hususan katika jiji
la Dar es Salaam
watu wengi hivi sasa hupenda kutumia usafiri huo ili kukwepa foleni na kuwahi
wanapokwenda.
Usafiri huo umesaidia kurahisisha mawasiliano katika sehemu
ambazo barabara hazipitiki kirahisi.Wakati hayo yanajiri magari madogo ya abiria yameathirika
kutokana na kuwepo usafiri huo kwani pamoja ni usafiri wa haraka sana na bado siyo ghali
kwa wasafiri ukilinganisha na bei za magari madogo kwa safari moja.
Vyombo hivyo vilianza kutumika baada ya Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
kupitisha sheria ya pikipiki na bajaji kutumika kubeba abiria.Pikipiki hizo zimekuwa ni sehemu ya ajira kwa vijana wengi,
kujipatia namna zao za kuishi na kuendesha familia zao.
Pamoja na faida hizo, pia kuna hasara nyingi zilizoletwa na
usafiri huo, ikiwa ni pamoja na ajali nyingi zinazotokana na pikipiki hizo na
majeruhi.Pamoja na kuwepo kwa usafiri huo lakini tayari umesababisha
ajali nyingi ikilinganishwa na magari na kupoteza maisha ya raia wasio na hatia
na wengine kupata vilema vya kudumu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uzembe
wa madereva hao.
Ajali na majeruhi vimefanya vijana waliokuwa wakitegemewa na
familia zao, kugeuka kuwa tegemezi badala ya kutegemewa, idadi kubwa ya
Watanzania wamepata vilema vya kudumu.
Madereva wengi nchini hawana leseni wala mafunzo ya
uendeshaji pikipiki kwa mujibu wa sheria ambao wengi walijiingiza huko kutokana
na kukosa ajira.
Uchunguzi uliofanywa unaonesha kuwa, idadi kubwa ya vijana
hao hawana mafunzo ya udereva na usalama barabarani. Ndiyo maana wengi wao
wanaendesha bila kufuata kanuni na sheria.
Pamoja na usemi wa ajali haina kinga, bado ajali nyingi
zinazotokea kwa uzembe zinazosababishwa na uharaka na kuacha kufuata sheria za
barabara zinavyosema na kuelekeza.
Tanzania kwa sasa ipo katika hatari ya kupoteza
nguvu kazi kutokana na ongezeko kubwa la ajali na kusababisha hali ngumu ya
maisha kwa wanaowategemea.
Ongezeko la magari na pikipiki nchini limekuwa tatizo kama siku za nyuma simba walivyokuwa wanajeruhi, kula
watu na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Mwaka 2008 kulikuwa na ajali za barabarani 17,451 na
kusababisha vifo 2,460 na majeruhi 16,982.
Mwaka 2009 kulikuwa na ajali 22,019 na kupoteza uhai wa watu
2,872, waliokufa 3,851 na waliojeruhiwa walikuwa 20,717.
Tofauti yake ilikuwa 4,568 sawa na asilimia 26.2.
Ajali zilizosababisha vifo ilikuwa 412 sawa na asilimia
16.7, waliokufa 1,011 sawa na asilimia 35.6 na waliojeruhiwa 3,735 ambapo ni
asilimia 22.
Mikoa iliyoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya ajali za
barabarani ilikuwa Dar es Salaam 6,538 na mwaka 2009 ilikuwa 9,312, Pwani
ilikuwa ya pili kwa ajali 1,315 lakini mwaka 2010 matukio ya ajali 1,239 na
kufanya Mkoa wa Arusha kuwa wa pili kwa idadi ya ajali 1,681.
Takwimu
zinaonesha kuwa, kadiri miaka inavyoenda ajali zinazidi kuongezeka pia badala
ya kupungua huku matumaini ya kumaliza tatizo hilo yakipotea.Mwaka 2010
zilitokea ajali 24,926 na kusababisha vifo 3,687, majeruhi 22,064 ambapo ajali
nyingi zilisababishwa na pikipiki.
Kutokana
na takwimu hizo, 2009, vyombo vya moto vilivyosajiliwa vilikuwa 624,909,
pikipiki zilikuwa 207,465 sawa na asilimia 33.1.
Ajali
za pikipiki pekee mwaka 2009 zilikuwa 3,945 na kupoteza nguvu kazi ya watu 385
na majeruhi 2,666.
Kutokana
na usafiri wa pikipiki kuwa mbadala kwa wananchi wengi tayari imesababisha
ongezeko la mahitaji yake kwa matumizi ya kila siku.
C h
a n g a m o t o k u b w a k w a waendesha pikipiki ni wizi ambapo mwaka 2009
ziliibwa 859 na 2010 idadi hiyo iliongezeka na kufikia 1,615 kutokana na
ongezeko la pikipiki kwa asilimia 87.9.
Kutokana
matukio haya kikosi cha usalama barabarani kinatakiwa kuangalia upya namna ya
kudhibiti ongezeko la ajali zinazosababishwa na pikipiki.
Kwanza waangalie leseni zao ili kuwabaini wasiokuwa nazo, pia
sheria za barabarani zifuatwe na wanaokiuka wachukuliwe hatua kali kinyume na
hivyo tutazalisha kundi la watu vilema.
Elimu
usalama barabarani inatakiwa kutiliwa mkazo ili kupunguza ajali hizo, pia
leseni zitolewe kihalali baada ya kupata mafunzo kama
madereva wengine.
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga kwa kushirikiana na watendaji
wake bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa vijana wengi wanaoendesha
pikipiki wanapata elimu ya usalama barabarani pamoja na kupata mafunzo ya
uendeshaji pikipiki.
Hivi
sasa katika maeneo mengi ya jiji vijana wengi wamejiajiri bila ya kuwa na elimu
yoyote ya usalama barabarani na pasipokuwa na leseni jambo ambalo limekuwa
likichangia kuongezeka kwa ajali na kuonekana sasa suala la ajali za pikipiki
ni ugonjwa.
Asilimia
kubwa ajali zinazotokea kila siku nyingi huwa zinatokana na pikipiki hivyo kuna
haja sasa ya kuboresha utoaji wa elimu ya usalama barabarani na kuhakikisha
kuwa vijana wanapata mafunzo ya udereva ikiwa ni pamoja na kuwafuata kwenye
vituo vyao ili kuinusuru nguvukazi ya taifa la
No comments:
Post a Comment