20 August 2013

NBC YAZINDUA HUDUMA YA KIFEDHA KUPIRTIA SARAFU YA CHINA




 Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma maalumu ya fedha za China katika Benki ya NBC, Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi.Mizinga Melu.


Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imezindua rasmi huduma mpya ya kifedha kwa kutumia sarafu ya China (Yuan) itakayowawezesha wateja na wafanyabiashara hapa nchini kufanya biashara kwa urahisi na wenzao kutoka China.

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo ya kipekee ana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu, alisema Benki ya Taifa ya Biashara imeamua kuja na huduma hiyo li kurahisisha biashara kati ya China na Tanzania. Melu alisema kwamba biashara kati ya Tanzania na China inakuwa kwa kasi sana na zinahitajika juhudi za lazima kuweza kufanikisha kwa haraka maendeleo kati ya nchi hizi mbili kupitia huduma za kibenki na kifedha.
Melu alisisitiza kwamba biashara kati ya China na Tanzania imekuwa katika siku za hivi karibuni ambapo kwa ujumla biashara ya Tanzania na China inafi kia dola za Marekani 2.15 billioni na hadi mwaka jana biashara kati ya nchi mbili ilifikia dola za Marekani 2.5 billioni na inatazamiwa kukua kwa asilimia 15 kwa mwaka. Kwa upande wake Balozi wa China hapa nchini, Dkt. Lu Youqing alisema China na watu wake hasa waishio hapa nchini wamepokea huduma hiyo ambayo itawawezesha wafanyabiashara kuweka na kutoa fedha zao kwa sarafu ya China
Dkt. Youqing alisema huduma za kifedha na kibenki ndiyo roho ya uchumi wanchi yeyote duniani katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa husika kwa kushirikisha taasisi za fedha. Balozi alisisitiza kwamba ushirikiano kati ya China na Tanzania unaendelea kukua kwa kasi katika nyanja zote za uchumi kama vile utalii, usafirishaji, bandari, gesi, umeme na sasa huduma hii ya kipekee ya kibenki. Dkt. Youqing alisema Serikali ya China itaendelea na juhudi zake za kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali pamoja na viwanda ili Watanzania waweze kuuza biashara zao nje ya nchi hasa China katika kukuza pato la ndani na fedha za kigeni

No comments:

Post a Comment