23 August 2013

MSHINDI AIRTEL AKABIDHIWA NYUMBA YA MIL.65/-Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Airtel, Bi. Beatrice Mallya (kushoto), akimkabidhi funguo ya nyumba iliyopo Kibada Dar es Salaam, mkazi wa Iringa, Bw. Silvanus Juma, ambaye ni mshindi wa shindano la 'Shinda Nyumba na Airtel Yatosha'. wakati wa hafla iliyofanyika Kibada jana

Na Frank Monyo
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imemkabidhi mshindi wa nyumba mkazi wa Iringa, Bw. Silvanus Juma, nyumba ya kisasa ya vyumba vitatu yenye thamani ya sh.milioni 65 baada ya kuibuka mshindi katika droo ya kwanza ya mwezi ya promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba
.Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya nyumba hiyo jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa mawasiliano Airtel, Beatrice Mallya, alisema nyumba hiyo imegharimu sh. milioni 65.
Alisema kuwa lengo ni kutoa maisha bora kwa Watanzania kupitia katika shindano la shinda nyumba na Airtel Yatosha."Mshindi amejinyakulia nyumba ya kisasa ya vyumba vitatu iliyopo Kigamboni Kibada kwa kushiriki kwenye promosheni ya Airtel yatosha na kununua vifurushi," alisema.
Alisema kuwa zimebaki nyumba mbili ambapo kila mwisho wa mwezi watatoa mshindi wa nyumba kupitia katika promosheni hiyo ambapo jinsi ya kushiriki ni kupiga *149*99# kisha anajiunga kwenye vifurushi vya Airtel yatosha
Naye mshindi wa nyumba Bw.Juma alisema amefurahi sana kwa kushinda zawadi ya nyumba kutoka Airtel kwani imembadilisha maisha yake."Hili shindano ni la kweli hakuna upendeleo wala ubaguzi hivyo ninawasihi Watanzania wenzangu ambao ni watumiaji wa Airtel kushiriki katika shindano hili," alisema

No comments:

Post a Comment