02 August 2013

MKE AMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA KISU KIFUANINa Elizabeth Joseph, Dodoma
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Jerida Jackson (33) mkazi wa Gulwe wilayani Mpwapwa kwa tuhuma na kumuua mume wake kwa kumchoma kisu kifuani
.Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani humo, David Misime alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 31, mwaka huu saa nane usiku nyumbani kwao Godegode Mpwapwa.
Misime alieleza kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya marehemu kumgombeza mtoto wake ndipo kukatokea mtafaruku baina yao hali iliyosababisha mtuhumiwa kumchoma kisu.
"Marehemu alimgombeza mtoto wake ndipo mtuhumiwa alihoji kwa nini anamgombeza mtoto baada ya kuhoji ndipo ukatokea mtafaruku baina yao na kumchoma mumewe kisu kifuani hadi kufikwa na mauti hayo," alisema Misime.
Aidha alimtaja marehemu kuwa ni Ramadhani Chiduo (41) ambapo Misime alitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi hali ambayo imekuwa ikisababisha madhara ikiwemo kifo na kuwataka kuwa na subira wakati inapotokea hali kama hiyo ya kutoelewana.

No comments:

Post a Comment