01 August 2013

MICHUANO YA NYERERE DAY OKTOBA 9



Na Ester Maongezi
CHAMA Cha Mieleka Tanzania (AWATA), kimeandaa michuano ya Nyerere Day, inayotarajia kufanyika Oktoba 9 mpaka 14 mwaka huu, baada ya kushindwa kufanikisha mashindano ya Mashujaa ya mwezi uliopita.Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa AWATA, Andrew Kapelela alisema michuano ya Mashujaa ilishindwa kufanyika kutokana na Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.

"Tulishindwa kuandaa michuano ya Mashujaa kutokana na kuwa katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa viongozi," alisema.Kapelela alisema mchakato wa uchaguzi huo ulikuwa mkubwa kwa kuwa chama walitakiwa viongozi watakaoiendesha AWATA kwa umakini.
Aliongeza kalenda ya michuano hiyo iliingiliana na uchaguzi huo, ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu kutokana na kwamba wanachama walihitaji mabadiliko ya kiutendaji.
Kapelela alisema michuano ya Nyerere Day itahusisha klabu zote zilizosajiliwa Tanzania Bara na kuzitaka kujiandaa kikamilifu.Mwenyekiti huyo alisema katika michuano hiyo ya Nyerere Day, bingwa atakabidhiwa kombe.

No comments:

Post a Comment