Na Goodluck Hongo
CHAMA cha Kijamii (CCK) kimemtaka Rais
Jakaya Kikwete na washauri wake kutafuta njia za kidiplomasia za kuzungumza na
Rais wa Rwanda, Paul Kagame ili kutafuta suluhisho la mivutano inayoendelea kwa
sasa kati ya pande mbili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa
vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mwenyekiti Taifa wa chama hicho,
Constantine Akitanda alisema kuwa kwa sasa kumekuwa na ushabiki mkubwa juu ya
uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda hivyo ni vema zikatumika njia za
kidiplomasia ili kutatua sababu za kurushiana maneno baina nchi yetu na Rwanda.
Alisema, kwa sasa baadhi ya watu wako
tayari na wameanza kushabikia vita au kutafuta suluhu kwa nguvu za kijeshi huku
wengine wakitamba kuwa tunaweza kuichakaza Rwanda kama tulivyofanya kwa Idi
Amin.
Alisema, mawazo ya namna hiyo ni ya hatari
na inawezekana yanatolewa pasipo kufikiria ambapo wale wanaotoa kauli hizo ni
lazima watambue kuwa vita si kitu kizuri kwani majeraha yake yanadumu kwa
vizazi na vizazi.
"Kwa wale ambao wamefika K a g e r a h a s a m a
e n e o yaliyoathirika na vita wanaweza kuona makovu yaliyobakia miaka zaidi ya
30, baada ya vita sasa tunawasihi viongozi wetu na vyombo vya habari kuepuka
kuchochea kauli za vita na uhasama kwa sababu tunaamini tu kuwa nchi yetu ina
uwezo wa kuipiga Rwanda na kusahau kabisa kuwa vita ni sehemu mbili kama vita
ya Uganda ilivyotufundisha," alisema Akitanda
No comments:
Post a Comment