05 August 2013

MBUNGE AIBUA MADAI MAZITO


N a S a m m y K i s i k a , Sumbawanga
MBUNGE wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilary, amesema nafasi yake ya ubunge imegeuka kero kutokana na baadhi ya wanasiasa wakongwe mkoani humo kupanga njama za kutaka kumuua.Aeshi amekuwa akitoa kauli hiyo kwenye mikutano mb a l imb a l i y a h a d h a r a anayoifanya katika ziara jimboni kwake. Mara ya kwanza kuzungumzia kuwepo kwa njama hizo ilikuwa katika mkutano uliofanyika katika Soko la Soweto kata ya Chanji
.Katika mkutano huo mbunge huyo aliwataka wananchi hao kumwombea na kumuunga mkono katika harakati zake za kuwatetea. "Ubunge wangu na msimamo ni mwiba kwa baadhi ya watu ambao hawapendi nipate mafanikio... wamekuwa hawalali na wanakesha ili waweze kunimaliza, nasema sintaacha kuwatetea wananchi wangu eti kwa sababu ya mtu fulani," alisema Aeshi.
Aeshi alisema ubunge wake umekuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi tangu achaguliwe mwaka 2010 ambapo alifunguliwa kesi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga ya kupinga ushindi wake.Alisema anaamini kuwa matokeo ya kufunguliwa kwa kesi ya kupinga ubunge wake yalitokana na shinikizo la baadhi ya wakongwe wa siasa ndani ya CCM mkoani Rukwa ambao tangu awali waliapa kuwa hawezi kupata ubunge, lakini kwa kudra za Mwenyezi Mungu alifanikiwa kuupata.
"Nina uhakika mimi napendwa sana na wapiga kura wangu, lakini wapo wazee ambao roho yao ni mbaya hawataki kuona hilo, sasa naomba niwaeleze kupitia mkutano huu kuwa mimi ndiye mbunge halali wa jimbo hili na nawaomba waniache niweze kushirikiana na wananchi wangu katika kuleta maendeleo ya jimbo hili," alisema na kuongeza.
"Kwa n i wa n a c h o umi a mimi kuwa mbunge ni nini?" Alihoji Mbunge huyo. Alisema licha kufunguliwa kesi za uchaguzi, miezi miwili baada ya kurejeshewa ubunge wake alipewa notisi ya siku 14 na mtu aliyemwita kuwa ni mwanasiasa mkongwe akimtaka kumwomba radhi ndani ya siku hizo vinginevyo atafikishwa mahakamani na kudaiwa fidia ya sh. milioni 800.
Al i s ema n o t i s i h i y o inadai kuwa Mbunge huyo amemdhalilisha mmoja wa wanasiasa wakongwe mkoani Rukwa kwa kumsema nje na kwenye vikao vya bunge lililopita mara baada ya kurejeshewa ubunge wake kuwa anamiliki nyumba nane mali ya Serikali ambazo alikodishiwa na Serikali na yeye akadaiwa kuzikodisha kwa wapangaji wageni kwa bei kubwa zaidi ya ile ya Serikali.
Aeshi alisema pamoja na notisi hiyo hataacha kuwatetea wapiga kura wake, kwani anafahamu wapiga kura wake wamekandamizwa katika maeneo mengi kwa miaka ya nyuma ikiwa ni pamoja na kudhulumiwa ardhi yao na kuongeza kuwa anawaomba wananchi hao kushikamana ili malengo yake ya kuwaletea maendeleo yaweze kufanikiwa.
Alisisitiza kwa muda mrefu wananchi wa mkoani Rukwa wamekuwa wakikandamizwa na hao watu, bahati mbaya hakukuwa na mtu wa kuwaeleza ukweli wao, lakini yeye ndiye suluhisho la mambo hayo, kwani haogopi na ataendelea kubomoa kila uovu wao wanaofanya.

No comments:

Post a Comment