Na Queen Lema, Meru
HALMASHAURI
ya Meru mkoani Arusha imeingia katika kashfa baada ya kutoa zabuni kwa
mkandarasi ambaye hana ofisi wala makazi maalumu kwa ajili ya kutekeleza miradi
ya maji katika baadhi ya vijiji hali ambayo imesababisha halmashauri hiyo kushindwa utoa
huduma bora ya maji kwa wananchi.
Hayo yamebainika mara baada ya Naibu Waziri wa Maji,
Binilith Mahenge baada ya kutembelea
baadhi ya miradi ambayo ipo chini ya halmashauri ambapo inadaiwa kuwa
halmashauri hiyo ni moja ya
halmashauri yenye vyanzo vingi vya maji lakini haina maji.
Akisoma
taarifa hiyo Mhandisi wa Maji wilaya hiyo, Maningo Mohamed alidai kuwa kwa
kipindi cha mwaka 2010 mpaka Aprili mwaka jana mkandarasi kutoka katika Kampuni ya Free World Co. Ltd aliingia mkataba na halmashauri
hiyo kwa malengo ya kufanya kazi lakini hakuweza kufanya kazi hiyo na badala yake
alikuwa anatoa visingizio vikiwemo vya kucheleweshewa bajeti ya Serikali kwenye sekta ya maji.
Mhandisi Mohamed alidai
kuwa mara baada ya kupewa mkataba mkandarasi huyo aliisumbua halmashauri kwa kuwa hakuwa na vifaa
lakini pia hata ofi si hali ambayo iliendelea kukwamisha miradi ya maji katika
wilaya hiyo hivyo kusababisha madhara makubwa ya uhaba wa maji. “Hi i k amp u n
i i l i p ewa mkataba lakini kwa bahati mbaya walidanganya kuwa wana ofi si
baada ya kuwafuatilia kwa undani tuliweza kujua na kutambua kuwa hana uwezo lakini tulishindwa
kumuondoa kutokana na sheria juu ya wakandarasi zinavyobana,”aliongeza mhandisi
huyo.
Akiongelea uhaba wa maji katika wilaya hiyo alidai kuwa linaendelea kukua
kwani kwa sasa lita zinazohitajika ni lita za ujazo elfu kumi na tano mia tano
wakati zinazozalishwa ni lita elfu sita tu kwa siku jambo ambalo linasababisha
uhaba mkubwa wa maji. Mhandisi Mohamed alibainisha kuwa uhaba huo wa maji unasababisha
madhara makubwa kwani wananchi wa wilaya hiyo wanalazimika kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta maji huku
shughuli za kila siku zikiwa zinakwama.
Awali Naibu Waziri wa Maji, Dkt. Mahenge alidai kuwa suala la mkandarasi
ambaye hana ofi si wala vifaa ni la kuhuzunisha kwani huo ni uzembe wa baadhi
ya watendaji wa halmashauri hiyo kushindwa kuwakagu wakandarasi kabla ya kuwapa
mikataba ya kazi. Dkt. Mahenge alisema kuwa suala hilo linatakiwa kuwa la
kwanza na la mwisho na uongozi wa Halmashauri unatakiwa kuomba hata
msaada kwa makandarasi wakorofi kwani wanasababisha hata miradi ya halmashauri ikiwemo
maji kukwama. Aliwataka hata viongozi wa Halmashauri nao kuhakikisha kuwa wanatafuta mbinu mbalimbali za kuongeza
kiwango cha uzalishaji wa maji kwani huduma ya maji iliyopo bado haiwatoshelezi
kabisa wananchi ingawaje wilaya hiyo ni moja ya wilaya hapa nchini yenye vyanzo
vya kutosha vya maji.
No comments:
Post a Comment