Na Rehema Mohamed
UWANJA wa Ndege wa Kima t a i f a wa J u
l i u s Nyerere (JNIA), umeendelea kukabiliwa na kashfa ya kupitisha dawa za
kulevya baada ya mkazi wa Dar es Salaam, kukamatwa jana na shehena ya dawa hizo
muda mfupi baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, kufanya ziara
uwanjani hapo
.Akizungumza
na waandishi Dar es Salaam jana, Dkt. Mwakyembe alimtaja mtu huyo kuwa ni Bw.
Jeremia Monyo (39) ambaye ni fundi mbao, mkazi wa Tegeta Mchakani.Alisema
kijana huyo mwenye rasta, alikamatwa akiwa na pipi 86 za dawa za kulevya aina
ya heroin na misokoto 34 ya bangi akiwa ameiweka katika begi dogo.
"Huyu
kijana alikamatwa saa 2:15 usiku kiwanjani hapo baada ya mzigo wake kutiliwa
shaka na wakaguzi wa mizigo ambao majina yao ni Grace Jonathan na Crantina
Jonathan, waliokuwa na mitambo ya kukagulia.
"Alikuwa
na hati ya kusafiria namba AB 202513 akienda nchini Italia kupitia
Zurich...nawapongeza hawa wakaguzi waliofanikisha kukamatwa kwake."Nitauagiza
uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAAA), uangalie namna ya kuwapandisha
vyeo au kuwaongeza mishahara," alisema Dkt. Mwakyembe.
Aliwataka
wakaguzi hao, kufanya kazi zao bila woga baada ya kuwataja majina yao hadharani
kwani wamefanya kazi nzuri hivyo wanastahili kupongezwa."Sihatarishi
maisha yao kwa kutaja majina hadharani, hakuna mwenye mkataba wa kuishi milele
na Mungu...hata mimi sitaishi milele hawa wamefanya kazi nzuri wanastahili
kupongezwa, kama hupendi joto usiingie jikoni," alisema.
Aliongeza kuwa, baada
ya kukamatwa kijana huyo kuanzia sasa watachapisha picha za watu wote ambao
watakamatwa uwanjani hapo wakipitisha dawa za kulevya.Dkt. Mwakyembe
alisema, pia wataanzisha utaratibu wa kukagua mizigo inayopitishwa katika
bandari zilizopo nchini kwa njia ya kisasa zaidi.
Katika hatua
nyingine, Dkt. Mwakyembe alisema baada ya ukaguzi wake uwanjani hapo, alibaini
tatizo la upitishaji dawa za kulevya katika uwanja huo halitokani na mitambo ya
ukaguzi bali watendaji wenyewe waliopewa dhamana.
A l i s e m a s u a l
a h i l o atalishughulikia na watendaji wote ambao watabainika kuhusika na
upitishaji wa dawa hizo, wataachishwa kazi bila kuoneana haya wala kuwaogopa.
"Kiwanja chetu
kina utaratibu mzuri wa kukagua mizingo na vifaa vipo vya kutosha ila tatizo ni
watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia majukumu, lazima hali hii tuidhibiti
kwani kiwanja hiki kinapitisha viongozi wakubwa," alisema.
Aliongeza kuwa, mbali na Watanzania kukamatwa na kilo 120 za
dawa hizo nchini Afrika Kusini, taarifa nyingine zinasema kuna Watanzania
wengine wawili wamekamatwa HongKong, China ambapo jambo hilo atalizungumzia
leo.
Tatizo lilipo ni rushwa bila kutoa mambo haya taendelea.Baadhi ya wafanyakazi hawana kiwango cha elimu kuweza kufanya hapo sijui wamepataje kazi hiyo.Tupo sisi watanzania tulio na elimu ya juu na ujuzi wa Hall ya juu lakini nafasi hizo hatupewi.
ReplyDeletekuna vijana wengi tupo magharibi huku na elimu ya kutosha na uchungu wa nchi yetu ,tupewe hata nafasi ya kujitolea hata kwa wiki 2 tukija likizo nyumbani,km ni lugha tunazijua,hatuogopi wageni ila tutaitetea nchi yetu,tupo km nurse,na wataalam wa computer,na biashara ,tunaweza kujitolea pia.na kuongeza camera hata kwenye viungo vya barabara za dar,arusha,na moshi na mwanza wajanja wanakopitia.tushirikisheni mtaona tofauti.
ReplyDeleteTatizo nchi yetu inaongozwa kwa mazoea na ndio maana mambo yanenda kienyeji tu.Nchi hii ina vijana wengi tu wenye nia ya kufanya kazi kwa kuwajibika lakini hawapati hizo kazi sababu nafasi zilizopo ni kwa ajili ya wale wanaojuana na wengine hata vigezo hawana.
ReplyDelete