12 August 2013

KIPLAGAT AIPA KENYA MEDALI YA DHAHABUMOSCOW, Urusi
BINGWA mtetezi wa mbio za marathoni kwa upande wa wanawake, Edna Kiplagat raia wa Kenya ametetea taji lake mapema juzi baada ya kushinda medali ya dhahabu.Kiplagat ameshinda mbio hizo kwa muda wa saa 2:25:44.

Valeria Straneo wa Italia alishika nafasi ya pili licha ya kuongoza kwa muda mrefu kwenye mbio hizo, lakini Kiplagat alianza kumuacha walipofika kilomita 40 na kumaliza mbio kwa zaidi ya sekunde 15 nyuma ya Straneo.
Kayoko Fukushi wa Japan alifanikiwa kushika nafasi ya tatu na kuchukua medali ya shaba.Hii ni medali ya kwanza ya Kenya ya dhahabu kwenye mashindano hayo ya Dunia, yanayoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF).

No comments:

Post a Comment