12 August 2013

32 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA COPA COCA-COLA



 Na Mwandishi Wetu
MAKOCHA 32 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani, wanashiriki kozi ya Copa Coca-Cola inayoanza leo jijini Dar es Salaam chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, kozi hiyo itakayomalizika Agosti 17 mwaka huu itafunguliwa saa 3:00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Msimbazi Centre.
Alisema washiriki wote tayari wameshawasili Dar es Salaam. Mkufunzi wa kozi hiyo ni Govinder Thondoo kutoka Mauritius.
Wambura alisema washiriki wa kozi hiyo ni Ahazi Kasegese (Mbeya), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Asuri Msakamali (Simiyu) na Bakari Kilambo (Kaskazini Pemba), Chacha Sambulo (Mara), Charles Rwezaura (Kagera), Daniel Sambala (Njombe), Dudu Haruni (Iringa) na Emmanuel Kapurata (Rukwa).
Aliwataja wengine kuwa ni Faki Makame Haji (Kaskazini Unguja), Fatawi Khamis Sheha (Kusini Pemba), Hamisi Mabo (Kigoma) na Hussein Maulid (Morogoro).
Wengine ni Issa Lugaza (Kilimanjaro), James Gaspar (Shinyanga), James Wambura (Arusha), Jomo Puccey (Lindi), Joseph Sihaba (Dodoma), Kelvin Haule (Ruvuma) na Kessy Abdallah (Tanga).
Makocha wengine ni Kessy Mziray (Mwanza), Menswi Mchwampaka (Kinondoni), Mohamed Kweka (Singida), Nurdin Gogola (Temeke), Pius Kamande (Rukwa), Ramadhan Abrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Ramadhan Mnyoti (Manyara), Raphael Ngeleja (Geita), Samuel Maokola (Ilala), Shaweji Nawanda (Mtwara) na Vuai Abdul Haji (Kusini Unguja).
Wambura alisema fainali za U15 Copa Coca-Cola, ngazi ya Taifa zitafanyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment