30 August 2013

KESI YA EPA YAKWAMANa Rehema Mohamed
UPANDE wa Mashtaka katika kesi ya kughushi na wizi wa zaidi ya sh.milioni 400 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) imekwama kusikilizwa kutokana na jopo linalosikiliza kesi hiyo kutokuwepo mahakamani.

Kesi hiyo inasikilizwa na Jopo la Mahakimu watatu ambao ni Projestus Kahyoza, Pamela Mazengo na Fransice Kabwe. Wakili wa serikali Veronica Matikila akishirikiana na Shadrack Kimaro jana aliieleza mahakama mbele ya Hakimu, Aloyce Katemana, kuwa kesi hiyo ililetwa kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa wa kesi hiyo.
Hata hivyo, Hakimu Katemana alizieleza pande zote za kesi hiyo kuwa jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo hawapo hivyo anaiahirisha hadi Septemba 24, mwaka huu. Kesi hiyo inawakabili mshtakiwa Farijara Hossein na Ajey Somani.

No comments:

Post a Comment