16 August 2013

JK KUZINDUA MFUKO WA WAJASIRIAMALINa John Gagarini, Kibaha
RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mfuko wa Wajasiriamali w a k a t i w a Tama s h a l a Wajasiriamali wilayani Bagamoyo mkoani Pwani litakalofanyika Septemba 19 mwaka huu
.Mwenyekiti wa tamasha hilo, Abdul Sharifu alisema kuwa tamasha hilo ambalo litafanyika kwenye ukumbi wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA).Sharifu alisema kuwa tamasha hilo litawashirikisha wajasiriamali zaidi ya 500 kutoka kwenye kata 22 za wilaya hiyo ili kuunda chombo cha pamoja kwa lengo la kuboresha shughuli zao.
Sharifu ambaye pia ni Meya wa mji wa Bagamoyo alisema kuwa tamasha hilo litaambatana na mafunzo ya siku tano kwa wajasiriamali hao."Wakufunzi watatoka kwenye sekta mbalimbali ikiwemo na Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) ili kuwapatia ujuzi wa kutengeneza bidhaa zao kwa viwango vinavyotakiwa kwenye soko la ndani na nje ya nchi," alisema Sharifu.
Aidha alisema kuwa changamoto kubwa aliyoiona kwa wajasiriamali wilayani humo ni ukosefu wa mitaji pamoja na upatikanaji malighafi na vifaa pamoja na pembejeo kwa wakulima.Aliongeza kuwa tamasha hilo litawahusisha wajasiriamali wadogowadogo wakiwemo mama lishe, wachonga vinyago, wafugaji wadogowadogo, wakulima, wafanyabiashara na vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali.  

No comments:

Post a Comment