22 August 2013

JK APANGUA MAKATIBU WAKUU Na Kassim Mahege
RAIS Jakaya Kikwete, amefanya mabadiliko ya makatibu wakuu 13 na manaibu 14 katika wizara mbalimbali nchini, hatua ambayo inalenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi Serikali.Mabadiliko hayo yalitangazwa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue Ombeni, alipozungumza na waandishi wa habari.

Katika mabadiliko hayo mapya waliokuwa makatibu wakuu wa wizara tatu watapangiwa kazi maalum. Alisema miongoni mwa makatibu wakuu wapya na manaibu wao miongoni mwao wametoka serikalini na wengine sekta binafsi na wengine kutoka wizara moja kwenda nyingine
Walioteuliwa na wizara zao kwenye mabano ni Florence Turuka (Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu), Joyce Mapunjo (Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki), Sihaba Mkinga (Katibu Mkuu, Habari, Michezo na Utamaduni) na Sofia Kaduma (Katibu Mkuu Kilimo na Ushirika)
Wengine, Dkt. Deo Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Afya), Uredi Mussa (Viwanda na Biashara), Dkt. Servacious Likwelile (Katibu Mkuu Wizara Fedha).Watakaopangiwa kazi nyingine baada ya kuondolewa kwenye nafasi zao ni Seth Kamuhanda, Kijakazi Mtengwa, Omary Chambo.
Manaibu Makatibu Wakuu wapya na ofisi zao kwenye mabano ni kama ifuatavyo, Angelina Madete (Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira), Regina Kikuli (Ofisi ya Waziri Mkuu), Zuber Samataba (Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Edwin Kiriba (Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) na Deodatus Mtasiwa (Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa -(Afya).
Wengine ni Dkt. Yamungu Kayandabila (Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika) Prof. Adolf Mkenda (Wizara ya Afya-Sera) Dorothy Mwanyika (Wizara ya Fedha- Fedha za Nje na Madeni), Rose Shelukindo (Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) Dkt. Selassie Mayunga (Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) Monica Mwamunyange (Wizara ya Uchukuzi) na Consolata Mgimba (Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi)
Aliwataja wengine kuwa ni Elisante Ole- Lazer (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo), Armantius Msole (Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki).Kwa upande wa waliohamishwa ni John Mngodo ambaye amehamishiwa Wizara ya Mawasiliano, Selestine Gesimba, amepangiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhandisi Ngosi Mwihava amehamishiwa Wizara ya Nishati na Madini.

No comments:

Post a Comment