07 August 2013

JESHI LABUNI TEKNOLOJIA MPYA UJENZI WA MAKAZI


Na Rehema Maigala, Bagamoyo
SERIKALI imeshauriwa kutumia teknolojia ya kujenga majengo kwa haraka (UBM) ili kuokoa gharama za ujenzi kwa taasisi zake zikiwemo shule, hospitali, kambi za jeshi ili kuharakisha maendeleo.Hayo yamebainishwa juzi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Juma Sippe wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa majengo ya shule ya awali ya mafunzo kijeshi Kihangaiko iliyopo Msata Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Alisema tekinolijia ya UBM imekuwa ikitumia mabati magumu bila ya kutumia nondo , nguzo za kushikia na mbao, na kwamba ujenzi huo hutumia siku kambi hizo na inachukua muda mfupi kumalizika tofauti na ujenzi kawaida ambao umezoeleka kwa watu wengi.
"Leo tumekuja kuangalia awamu ya pili ya ujenzi wa kambi hii ikiwamo mabweni ya makuruta wetu ambao watakuwa katika mafunzo,"Naye, Mhandisi wa chuo hicho cha mafunzo, Julias Msangi alisema, licha ya awamu ya kwanza kukamilika kwa wakati lakini kumekuwa na changamoto ikiwamo ubebaji wa mashine hizo kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Alisema kwa kutumia UBM wanaweza kujenga mabweni matatu kwa siku sita ukiachilia mbali jengo kubwa la utawala ambalo wamelijenga ujenzi wa kawaida wakichanganya teknolojia hiyo ambapo mradi huo wa awamu ya pili unatarajia kutumia zaidi ya sh milioni 800 kama kianzio

No comments:

Post a Comment