16 August 2013

IUCEA LAANZISHA USHIRIKIANO VIWANDA NA WASOMI Na Isaac Mwangi, EANA
BARAZA la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki (IUCEA) limeanzisha ushirikiano na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) katika juhudi mpya za kuunganisha viwanda na wasomi katika kanda hiyo.T a a s i s i h i z o m b i l i , zinazofanyakazi kwa ushirikiano wa karibu na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa pamoja wameandaa Kongamano na Maonesha ya Wosomi na Sekta Binafsi 2013 yatakayofanyika baadaye mwaka huu.

Tukio hilo linatarajiwa kufanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Kenyatta, nchini Kenya Oktoba 23-25.
Akihutubia mkutano wa waandishi wa habari mjini Nairobi Kenya, baada ya, maandalizi ya kongamano hilo, Katibu Mtendaji wa IUCEA, Prof. Mayunga Nkunya alisema watu wapatao 300 wanatarajiwa kushiriki katika kongamano hilo mwaka huu.
Huku ikitarajiwa kuvileta pamoja vyuo vikuu 102 kutoka Afrika Mashariki yote, kongamano hilo linatarajiwa kuvutia wengi kutoka maeneo mbalimbali duniani. Taasisi binafsi zipatazo 50 zinatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo la siku tatu."Kongamano hili litawaleta pamoja wasomi na sekta binafsi ili kuzalisha kile kinachotakiwa kwenye soko,'' Prof. Nkunya alisema na kuongeza kuwa vyuo vikuu havina budi kufundisha kile kinachohitajika na siyo kufundisha tu bila maana yoyote".
"Mgando wa mawazo hauna budi kubadilika katika mazingira mapya ya kiuchumi tuliyonayo...vyuo vikuu ni lazima vifanye kazi kwa pamoja na sekta binafsi,'' alisisitiza.Hili litakuwa kongamano la pili kuandaliwa na taasisi hizo mbili katika juhudi za kuunganisha elimu ya juu na viwanda, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki limeripoti

No comments:

Post a Comment