16 August 2013

HIFADHI YA CHAKULA KUNUNUA MAHINDI TANI ELFU 50Na Cresensia Kapinga, Songea
WAKALA wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa mkoani Ruvuma (NFRA) wanatarajia kununua tani 50,000 za mahindi katika msimu wa mavuno wa mwaka huu na tayari wameshanunua tani 21,000 za mahindi ndani ya wiki tatu tangu msimu ulipofunguliwa.

Akizungumza ofisini kwake jana na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw.Said Mambungu alisema kuwa mwaka huu wakulima wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kuuza mahindi yao kwenye hifadhi ya chakula kutokana na bei iliyopangwa na Serikali kuwa nzuri tofauti na za walanguzi.
Alisema kuwa lengo la Serikali kununua tani elfu 50 za mahindi na kwamba mwaka huu kasi ya ununuzi imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana ambapo lengo lilikuwa kununua tani elfu 50 walinunua tani elfu 26 tu ambazo tayari zimeuzwa ndani ya nchi na zingine zimeuzwa nje ya nchi.
Al i s ema k uwa t a y a r i wameshapata fedha za ununuzi wa mahindi kwa awamu ya kwanza ambazo zimeisha na tayari wameletewa tena kiasi cha sh.bilioni 3 na kwamba wananunua kwa kilo moja ya mahindi sh.500 kiwango ambacho ni halali na kitawasaidia wakulima kuinua kipato chao.
Ha t a h i v y o amewa t a k a wakulima kuyauza mahindi yao kwa wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa kwani wanahifadhi mahindi kitaalamu na kwa sababu ni hifadhi ya taifa itawasaidia pindi watakapoishiwa chakula watauziwa kwa bei nafuu tofauti na wafanyabiashara wengine.
" T u m e w a p i g a b a o wafanyabiashara ambao kazi yao ni kuwalalia wakulima kwa kununua mahindi bei ya chini lakini hata hivyo Serikali haimzuii mfanyabiashara yeyote yule kununua mahindi kwa wakulima isipokuwa wafuate bei ya halali iliyopangwa na Serikali na atakaye nunua mahindi kwa bei ya chini ya sh.500 akibainika atachukuliwa hatua za kisheria," alisema Mwambungu.
Mwambungu ameonya vitendo vya baadhi ya wakulima kutokuwa waaminifu pindi wanapopeleka mazao yao kwenda kuyauza mara nyingi wanachanganya na takataka kitendo ambacho amesema si cha kiungwana hata kidogo.
Hata hivyo ametoa rai kwa wakulima kutumia vizuri mapato wanayopata ili yaweze kusaidia kuinua kiwango cha maisha ya familia ikiwemo kusomesha watoto na baadhi ya wanaume wenye tabia ya kuchukua mapato na kufanyia mambo nje ya familia zao ni vyema wakajiepusha kwa kuzibadilisha familia zao.
Aidha watu zaidi ya 500 tayari wamepata ajira mbalimbali kwenye hifadhi hiyo ya chakula ikiwemo ya kuchekecha mahindi na zingine ambazo zitasaidia kuinua viwango vya maisha yao ya kila siku tofauti na walipokuwa hawana kazi.

No comments:

Post a Comment