Na Suleiman Abeid, Simiyu
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti,
amelipongeza Kanisa Katoliki Kigango cha Kilole, kwa kumwalika Waziri wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi
wa kanisa hilo na kuwaacha viongozi ambao si waadilifu ambao wangetoa fedha
zinazotokana na mikono michafu.Mabiti alitoa
pongezi hizo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi
wa Kanisa hilo wilayani Busega. Alisema Sitta ni kiongozi mwadilifu asiye na
kashfa yoyote serikalini na ni mfano wa kuigwa
. "Napongeza
uongozi wa kanisa hili kwa kumchagua Sitta kuongoza harambee hiyo badala ya
kuchagua viongozi ambao si waadilifu ambao wangetoa fedha zinazotokana na
mikono michafu," alisema.Akitoa historia
ya Sitta kwa waumini waliohudhuria harambee hiyo, mkuu huyo alisema mwaka 1977
Sitta akiwa naibu waziri wa mawasiliano nchini ndiye aliyefanikisha uanzishwaji
wa vyombo vipya vya umma nchini baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Alisema Sitta ndiye
aliyejenga barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma kwa kiwango cha lami, daraja la
Salander, Shirika la Reli (TRC), Shirika la Ndege (ATC) ikiwemo pia bandari ya
Dar es Salaam na kwamba ni miongoni mwa wabunge waliofanikisha kuchaguliwa
kwake (Mabiti) kuwa mbunge mwaka 1985.
“Hata daraja la Kirumi kule mkoani
Mara, daraja la Salander Dar es Salaam, barabara ya Makambako hadi Songea zote
hizi zilijengwa na Sitta, sasa niwaulize hapa katika kipindi chote hicho ni
nani miongoni mwenu aliyewahi kusikia huyu bwana akituhumiwa kwa kashfa yoyote
ile, asimame hapa ataje,” alihoji Mabiti na kushangiliwa na wananchi.
Alisema kanisa linapochagua mgeni rasmi
kuongoza harambee linatakiwa lichague mtu msafi na kwa kuwa kanisa la Mungu
halifai kujengwa kutokana na fedha chafu na kwamba Sitta ni miongoni mwa
viongozi wasafi na waadilifu nchini hali ambayo ilisababisha hata yeye (Mabiti)
kukubali kushiriki katika harambee hiyo.
“Kanisa linapochagua mgeni rasmi kuja
kwenye harambee kama hii lisiite kiongozi kama kiongozi, kuna wengine wana
fedha haramu ambazo hazifai kujenga kanisa la Mungu, mheshimiwa Sitta ni
kiongozi safi na ndiyo maana hata akina sisi (Mabiti) tumekuja, vinginevyo
nisingekuja, ningetoa udhuru, lakini niliposikia ni yeye (Sitta) nikaja,”
alisema Mabiti.
Kwa upande wake Sitta akizungumza
katika harambee hiyo aliwapongeza wananchi wote waliojitokeza katika shughuli
hiyo ambapo alisema yeye binafsi ameridhishwa na mwitikio waliouonesha na
kufafanua kuwa baadhi ya wenzake ambao wangeshiriki katika harambee hiyo
walipata udhuru na kwamba watakwenda kwa wakati wao.
“Wenzangu ambao ningekuja nao hapa leo
wamepata udhuru, wengine wako katika ziara ya Rais kule Kagera na mwingine yuko
Zimbabwe kufuatilia shughuli za uchaguzi mkuu unaofanyika nchini humo, lakini leo
siyo mwisho, huu ni mwanzo, tutakuja tena, naamini tutaendesha harambee babu
kubwa, nitamleta na Waziri Mkuu Pinda,” alisema Sitta.
S i t t a a l iwa t a h a d h a r i s h
a Watanzania wanaopiga kelele wakilalamikia kutoyaona maisha bora kama walivyoahidiwa
na serikali ya CCM kwa kueleza kuwa maisha bora hayawezi kuwadondokea watu
wasiojishughulisha na kufanya kazi yoyote ya kuwaingizia kipato.
Kuhusu suala la ufisadi, waziri Sitta
alisema Watanzania wanapaswa kujitenga mbali na watuhumiwa wanaobainika kuj
ihusishan avitend ovya ufi sadi nakwamb aw apob aadhiyaoambao hivi
sasawanahangaikakupitakilakona wakisambaza fedha.
Zaidi ya shilingi milioni 120 zilik usanywa
katikaharambeehiyoambayoilikuwa imelenga kuk usany akiasi chash. milioni
270hukuw aziriSitta akichangiash. milioni tatu na mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mabiti aliyechangia sh. milioni moja
No comments:
Post a Comment