MKURUGENZ I Mt e n d a j i wa H a l m a s h a u r i ya Wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa, Paul Ntimka amelipongeza gazeti la Majira kwa kuandika habari
nyingi za maendeleo wilayani Mufindi.Hali ambayo imesababisha wananchi kujua shughuli za maendeleo ambazo
zinafanywa na Serikali ya wilaya katika maeneo ya vijijini huku akivitaka
vyombo vingine vya habari kuiga mfano wa Majira katika kuandika taarifa za
ukweli.
Taarifa ambazo zinalenga maendeleo ambayo Serikali inafanya hususan
katika maeneo ya vijijini ikiwemo miradi ya maji, barabara, umeme, kilimo,
misitu, afya na ujasiriamali.
A k i z u n g u m z a j a n a kwenye Baraza la Madiwani lililofanyika
kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Ntimka alisema gazeti hili
ni mfano wa kuigwa hivyo madiwani, maofisa watendaji na wenyeviti wa vijiji
wanatakiwa watoe ushirikiano wa kutoa habari.
Alisema kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi kuwakimbia
waandishi wa habari wakati wanapofika kuzitafuta habari nzuri na zinazohusu
maendeleo.
"Viongozi wa vijiji, madiwani, watendaji wa vijiji, kata na tarafa
ninawaomba toeni ushirikiano mkubwa kwa vyombo vya habari, pale ambapo habari
katika kijiji chako zinaandikwa kuhusiana na maendeleo ambayo yamefanyika ni
sifa kwako wewe kiongozi, Serikali na wananchi wanatambua kuwa kumbe Serikali
yao inawafanyia nini na siyo kuwakimbia, kwa nini mnawaogopa waandishi wa
habari, wana malengo mazuri na taifa letu," alifafanua Mkurugenzi huyo.
Aliongeza kuwa, gazeti la Majira katika kuandika habari zake
wanahakikisha wanajiridhisha katika vyanzo vyote vya habari wakiwemo wananchi,
viongozi ngazi za vijijini, kata, tarafa na wilaya suala ambalo limesababisha k
u w a n a u m o j a n a mshikamano kiutendaji kwa kuwa na mfumo wa habari zenye
mtiririko sahihi kutoka ngazi za chini hadi juu.
K w a u p a n d e w a k e Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi, Peter Tweve aliunga mkono kauli ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mufindi, Paul Ntimka na kuongeza kuwa ili vijiji, kata, tarafa na wilaya
iweze kutambulika m a t a t i z o y a k e n a maendeleo yake kunatakiwa kuwepo
ushirikiano mkubwa baina ya viongozi wa ngazi zote.
Sambamba na
vyombo vya habari na siyo kukimbiana na kushindwa kupeana habari.
Mwenyekiti huyo
alisema kuwa, miradi mingi ambayo imekuwa ikifanywa na Serikali katika maeneo
ya vijijini inatakiwa ijulikane na siyo kuiweka kiusiri ambapo alisema kuwa,
gazeti la Majira limekuwa likitoa habari za maendeleo na kufukua habari zote
zenye kuwatofautisha wananchi na Serikali ili kuhakikisha kunajengwa umoja
makini kati ya wananchi na Serikali yao.
Alisema kuwa,
katika ulimwengu unavyokwenda k w a s a s a w a n a n c h i wanatakiwa waambiwe
wazi kuhusiana na maendeleo a m b a y o s e r i k a l i y a o inawafanyia na
siyo kuficha ficha suala ambalo wananchi baadaye wanaweza kuanza kuhoji
kulikoni huku vyombo vya habari vikifuatilia mashaka hayo wakati kama
ushirikiano ungekuwepo mambo yangeenda vizuri.
No comments:
Post a Comment