23 August 2013

DKT. MWAKYEMBE AONYA WATUMISHI. Na Grace Ndossa

WAZIRIwa Uchukuzi Dkt. Harris onMwakyembeamesemawa tumishi watakaoshin dwakutekelezaMpangowaSerika liwa kupata Matokeo Ma kubwak waHaraka(BRN),ajian daekufuk uzwak azi kwani ha kunamtu mishiambay eanaajirayakudumu ambayo haiwezi kugu swa
.Dkt.Mwakyem be a liong ezaajiraza watu mishi haosiyojiwekwa mba haliw ezikutokail awa takwendana watuwan aokidh ik asiinayotakiw akatikaSerika li.Kau li hiyoaliitoa Dar es Salaam jan a, alipo kuw aaki fun guaseminayawadauwase ktayausa firishaji kwa watumishi wa wizara hiyo.Alisema,m pango huo waSerik ali unaangali amatokeoha lisinasi ubabai shajina k wambak ilamtumishiatapi mwakutokan ana kile anachokifanya.
Alisema, watumis hi wa sekta ya Uchu kuziwa natakiw a k ufanyak azi kwakufua tauhitajiwaserikal iwakutekelez am pango waMatokeoMakubwan aambayeanao na hawezi ajion do emwenyewe na akatafute kaziyak ufanya.Dkt.Mwakyembe alisemampango huo unalengakuifungua KandayaK atikatikasualala uchuku zi n awan atarajia kufuf uareli ilikuon dokananaus afirish aji wami zigomizito kw anjiayabarabara, ambazo ni hatari kwa barabara.

"Mtumishi atakayeshindwa kutekeleza mpango wa Serikali wa kupata matokeo makubwa kwa haraka (BRN), ajiandae kufukuzwa kazi kwani hakuna mtumishi ambaye ana ajira ya kudumu ambayo haiwezi kuguswa, ajira zenu siyo jiwe kwamba haliwezi kutoka, tutakwenda na watu wanaokidhi kasi tuitakayo.

"Hatuwezi kuendelea na aibu hii ya kusafirisha tani 200,000 tu kwa mwaka, lengo letu ni kuhakikisha tunafikisha tani milioni tatu kwa mwaka ili pamoja na mambo mengine tuokoe barabara zetu,” alisema Dkt. Mwakyembe.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Rais ya kufuatilia Matokeo ya Mpango wa BRN, Omary Issa alisema tayari wamekwishaanza ufuatiliaji ambapo kila Jumatatu ya kila wiki wizara zilizopo kwenye mpango huo zinalazimika kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wa Rwanda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam alisema, Tanzania haiwezi kuyumbishwa na hatua ya nchi hiyo kuacha kupitisha mizigo yake katika Bandari ya Dar es Salaam, badala yake inajikita zaidi kuimarisha sekta ya uchukuzi.

Alisema, ni mwendawazimu pekee ambaye anaweza kupitisha mizigo Bandari ya Mombasa kwenda Kigali, Rwanda kutokana na umbali mrefu uliopo kwani kutoka Dar es Salaam kwenda Rwanda ni karibu zaidi.

No comments:

Post a Comment