30 August 2013

ASKARI JWTZ AUWAWA GOMANa Rehema Mohamed
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Khatibu Mshindo, ambaye ni miongoni mwa wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani Mjini Goma, nchini Kongo (DRC), ameuawa baada ya kuangukiwa na bomu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya jeshi hilo, ilisema Meja Mshindo, aliangukiwa na bomu akiwa na askari wenzake Agosti 28, mwaka huu."Wanajeshi wengine walijeruhiwa katika tukio hilo, Meja Mshindo alikuwa miongoni mwa majeruhi lakini alifariki dunia wakati akikimbizwa hospitali," ilisema taarifa hiyo.
Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu ambapo hali zao zinaendelea vizuri (bila kueleza idadi yao).
Wanajeshi wa JWTZ wanashiriki katika Operesheni za Umoja wa Mataifa Mjini Goma, wakiendelea kutekeleza majukumu yao ya kulinda amani kama wanavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa, DRC lijulikanalo kama MONUSCO.Taarifa hiyo iliongeza kuwa, MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuusafirisha mwili huo hadi Tanzania

1 comment:

  1. Watanzania,
    Hiki kifo cha askari ni sababisho la rais wa Rwanda ambaye anafadhili vikundi vya waasi nchini DRC. Kama Kagame anasikia basi aache kufadhili watu wanaohatarisha usalama wa nchi au wa watu wengine.

    Aidha, serikali yetu ya Tanzania iangalie jinsi gani watoto wa askari wanaofia vitani watakavyotunzwa kwa kupatiwa mahitaji muhimu.

    Tanzania tuzidi kwa umoja wetu kulaani mauaji na nchi zinazowafadhili waasi.

    ReplyDelete