19 August 2013

25 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI TFF



 Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya wanamichezo 25 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27, mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura ilieleza kuwa fomu hizo zilianza kutolewa Agosti 16 mwaka huu ambapo wawili wamechukua nafasi ya Rais.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa wadau wengine wawili wamechukua fomu za Makamu wa Rais wakati waliobaki wanaomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.Waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea urais ni Jamal Malinzi na Omari Musa Nkwarulo wakati umakamu wa rais hadi sasa umewavutia Wallace Karia na Ramadhan Nassib.
Waliochukua fomu za ujumbe ni Athuman Kambi, Charles Komba, Davis Mosha, Elias Mwanjala, Eliud Mvella, Epaphra Swai, Farid Nahdi, Hussein Mwamba, Jumbe Magati, Kamwanga Tambwe na Khalid Mohamed.
Wengine ni Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir, Omari Walii, Samwel Nyalla, Shaffih Dauda, Stanley Lugenge, Twahir Njoki, Vedastus Lufano, Venance Mwamoto na Wilfred Kidao.Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu aliyechukua fomu mpaka sasa ni Hamad Yahya anayeomba kuteuliwa kugombea nafasi ya uenyekiti. Fomu za maombi pia zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ambayo ni www.tff.or.tz mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni saa 10 kamili jioni ya Agosti 20 mwaka huu

No comments:

Post a Comment