19 August 2013

CANAVARO APONDA NDUMBA YANGA,SIMBA Na Amina Athumani
NAHODHA wa timu ya Yanga Nadiri Haroub 'Canavaro' amewaasa wachezaji wenzake wa klabu yake na ya Simba kutoamini ushirikina katika soka, lakini uwezo wao na juhudi zao ndiyo zitasaidia timu zao kufanya vyema hasa katika Ligi Kuu Tanzania bara.

Canavaro alisema jana wakati wa semina elekezi kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu na Daraja la Kwanza iliyoandaliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kwa timu za mkoa huu, ambapo semina hiyo ililenga kutoa mafunzo ya sheria 17 za soka, jinsi ya kuripoti habari za klabu na Kamati ya Ufundi.
Alisema masuala ya ushirikina waziachie kamati za ufundi wao, wajikite katika kuhakikisha wanajituma na kuzingatia mafunzo ya walimu ili kuweza kuhakikisha wanafanya vyema katika timu zao na sio kuingilia masuala yasiyowafaa.
"Kama kuna masuala ya ndumba yapo na yataendelea kuwepo kwani yameshajengeka katika fikra za watu, lakini sisi wachezaji hasa Yanga na Simba tuzingatie mazoezi na kujituma, hayo masuala mengine tuwaachie wao wanaofanya," alisema.
Alisema kwa upande wa Yanga wao hawajashuhudia mambo hayo na wao kinachowasaidia kufanya vizuri ni mazoezi na kujituma na ndiyo maana timu yao imekuwa ikifanya vizuri siku zote na viongozi hawajihusishi katika masuala hayo

No comments:

Post a Comment