19 August 2013

WATANZANIA WAANGUKIA PUA NCHINI MOSCOW Na Amina Athumani
WA N A R I A D H A w a Tanzania waliokwenda kushiriki mashindano ya Dunia kwa upande wa mbio ndefu za Marathon, wameshindwa kufanya vizuri katika michuano hiyo, huku mwanariadha Fautine Mussa akishika nafasi ya 34 na Msenduki Mohamed kuambulia nafasi ya 39

Mashindano hayo yalifanyika katika uwanja wa Luzhniki Stadium katika jiji la Moscow nchini Urusi ambapo yalikuwa na mbio mbalimbali kuanzia mita 100 hadi mbio ndefu za Marathon.
Mussa alimaliza mbio hizo akitumia muda wa saa 2:20:51 wakati Msenduki akimaliza kwa kutumia muda wa saa 2:24:20.
Michuano hiyo iliyoshirikisha wanariadha kutoka nchi mbalimbali, ilikuwa na upinzani mkali huku Uganda iking'ara kwa kutwaa medali ya dhahabu katika mbio ndefu.
Kutokana na matokeo hayo Tanzania bado imeendelea kufanya vibaya katika michezo ya Kimataifa ambapo mbali na mashindano hayo ya Dunia Mussa na Msenduki pia hawakuweza kufanya vizuri katika mbio hizo katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika mwaka jana.

No comments:

Post a Comment