Na Rashid Mkwinda, Mbeya
ASILIMIA 7.7 ya watoto walio chini ya
umri wa miaka mitano ndio waliosajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa kati ya
asilimia 14 ya watoto wote nchini ikiwa ni asilimia 23 tu ya wananchi wote ambao
wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa nchini.
Kwa mujibu wa
taarifa ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) katika uzinduzi wa
mfumo mpya wa usajili wa vizazi kwa watoto waliochini ya miaka mitano, ni
kwamba takwimu hizo zimekuwa haziridhishi kwa kutambua umuhimu wa usajili na
utunzaji wa kumbukumbu muhimu za vizazi mwaka 2011.
Akizungumza
katika uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili kwa watoto waliochini ya miaka mitano
kwenye viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Vicent Mrisho alisema kudorora
kwa mfumo wa usajili kumechangia serikali kukosa takwimu muhimu kwa mipango ya
maendeleo ya Taifa.
Mrisho alisema kuwa kutokana na kuwepo
kwa takwimu zisizoridhisha za kumbukumbu za vizazi mwaka 2011 RITA kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali ilibuni mkakati wa usajili wa watoto wa umri
wa chini ya miaka mitano wenye lengo la kuboresha hali ya usajili nchini na
kuweka kipaumbele kwa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.
Alisema kuwa kundi hili la watoto chini
ya miaka mitano lilichaguliwa kwa sababu ya kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa
anapata cheti kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani na pia kundi ambalo hutumika
kama kipimo katika mkataba wa Kimataifa kuhusu haki za Mtoto na Malengo la
Milenia.
Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu
Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda alisema mfumo mpya wa usajili ni sehemu ya ugatuaji wa madaraka
kupeleka huduma katika ngazi ya serikali za mitaa.
Alisema awali usajili ulikuwa
ukifanyika katika ofisi za Mkuu wa wilaya hali ambayo ilichangia kujitokeza kwa
idadi ndogo na hivyo kuleta changamoto inayohitaji mipango mahsusi na kwamba
mkakati huu utatoa suluhisho kwa mpango wa maendeleo ya Taifa.
Uzinduzi huu wa usajili wa vizazi na vifo utafanyika katika
mikoa mitano ya Mbeya, Mwanza, Simiyu, Shinyanga na Geita ambapo kwa mkoa wa
Mbeya kutakuwa na vituo 333 vya usajili katika ngazi ya ofisi za watendaji wa
kata na vituo vya afya.
No comments:
Post a Comment