31 July 2013

WATABIBU WAIOMBA TFDA KUCHUNGUZA UPYA MAFUTA YA UBUYU



 Na Heri Shaaban
WA T A B I B U wameiomba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kufanya uchunguzi upya na wa kina wa mafuta ya karafuu, alizeti, mwarobaini na mlonge ili kuondokana na hofu iliyopo kwa jamii. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kituo cha Tiba, Lishe na Ushauri na Vipodozi Asili cha Tabata, Dkt. Othman Shem alisema sababu ya ombi hilo ni kutokana na mkanganyiko wa mafuta ya ubuyu kuwa si salama kwa matumizi
. Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na taarifa ya TFDA kwa umma ya kuzuia mafuta ya ubuyu kwa madai kuwa yana madhara kiafya wakati yametumika zaidi ya miaka saba. A l i s ema k u w a i l i kuondokana na mkanganyiko huo ni vizuri Wizara ya Afya, TFDA na Taasisi ya Utafiti Tanzania (NIMRI) kuyafanyia uchunguzi mafuta hayo na kutoa taarifa sahihi kwa umma.
"Matumizi ya mafuta ya ubuyu yameanza kutumika zaidi ya miaka saba iliyopita na jamii na ulimwengu wanayatumia katika kipindi hicho hayakuonekana kama yana madhara kwa binadamu kwanini leo serikali izinduke usingizini na kuona hayafai," alihoji Shem.
A l i s e m a k a m a imegundulika mafuta ya ubuyu si salama kutokana na uchunguzi pia ni vizuri sasa wakafanya uchunguzi wa mafuta ya karafuu, mlonge, alizeti na mwarobaini ambavyo vimetumika muda mrefu. Pia wameomba kuzingatia suala la vifaa kwani kuna uwezekano wa vifaa vya awali kuwa na kasoro hivyo ni vizuri mafuta ya ubuyu yakapimwa upya.
" H u e n d a m a f u t a waliyotumia TFDA kuyapima labda yalikuwa yamevunda ndio maana wamegundua kutofaa kiafya lakini nchi zaidi ya 100 mpaka sasa wanatumia mafuta hayo," alisema.. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Sefu Rashidi alisema taarifa imechelewa kutolewa kwa umma kutokana na kuyafanyia uchunguzi taratibu na kuonekana kuwa na madhara ya kansa.

No comments:

Post a Comment