05 July 2013

WANAOINGIZA MIFUGO KIHOLELA KUSAKWANa Stella Shoo, Morogoro
VIONGOZ I wa d i n i , w a z e e m a a r u f u pamoja na madiwani wametakiwa kuwafichua watu wanaowaruhusu wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye vijiji wilayani Kilosa katika Mkoa wa Morogoro kwakuwa mifugo hiyo imekuwa ikiongeza na kuchochea migogoro.
Akizungumza mjini Kilosa juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema tatizo la mapigano ya wakulima na wafugaji limekuwa kero wilayani humo na imefikia wa k a t i v i o n g o z i wa d i n i wakishirikiana na wazee maarufu kuwafichua wanaoingiza mifugo kiholela ili kukomesha tatizo hilo.

"Tatizo la wakulima na wafugaji limekuwa kero, mifugo inazidi kuongezeka kila siku, sasa ndugu zangu tuambiane hii mifugo inatoka wapi na nani anaikaribisha, nawaombeni tushirikiane ili kutokomeza tatizo hili," alisisitiza Shilogile.

Akizungumzia vurugu za siasa zinazojitokeza wilayani humo hasa katika Tarafa ya Ruaha, Shilogile alisema anachukizwa na matukio hayo na yuko tayari kuhamia Ruaha ili kutafuta amani kwa kuwa nchi ya Tanzania na hakuna kiongozi yeyote atakayekubali kuona mkoa wake unaharibiwa na baadhi ya makundi ya watu wasiopenda maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kilosa, Break Magessa aliwaambia viongozi wa wilaya pamoja na wazee maarufu wilayani humo wazidi kuwaelimisha wananchi na jamii inayowazunguka juu ya utulivu na amani na kuwa Jeshi la Polisi wilayani humo halitamvumilia yeyote atakayekiuka na kuvunja sheria kwani atawajibishwa mara moja.
"Tunawategemea sana ninyi mkielimisha jamii kuwa Jeshi la Polisi liko kwa ajili ya wananchi na inapotokea mtu kukiuka sheria, basi tupeane taarifa ili tuweze kutokomeza uhalifu katika wilaya yetu," alibainisha Magessa


No comments:

Post a Comment