Na Esther Macha, Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya imewaagiza viongozi
wa ngazi za vijiji na kata kutoa elimu kwa wananchi ya ufugaji nyuki ili kuweza
kujiongezea kipata kitokanacho na asali ili kujikwamua kiuchumi kutokana na
mradi huo kutogharimu fedha nyingi.
Mwito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dkt. Norman Sigala wakati wa kilele cha maadhimisho ya
siku ya Serikali za Mitaa yaliyofanyika katika Kata ya Swaya jijini humo ambapo
kauli mbiu ya mwaka ni amani, uadilifu, uwajibikaji ni nyenzo muhimu katika
mchakato wa katiba mpya na ustawi wa Serikali za Mitaa.
Alisema kuwa urinaji wa asali hauhitaji
pembejeo za kilimo bali ni maandalizi ya kuwepo na mizinga na kwamba kwa
kipindi hiki zao hilo limekuwa na faida kubwa ambapo kuna uwezo wa kumwingizia
mrinaji zaidi ya shilingi 250,000 kwa mzinga mmoja.
"Ndugu zangu wananchi miradi ni mingi
ya kujikwamua kiuchumi na si kutegemea kilimo pekee na kwamba ufikie wakati
sasa kuamka na kujikita katika ufugaji wa nyuki na Serikali itakuwa bega kwa
bega na nyinyi hususan kuwafikishia wataalam wa ufugaji wa nyuki,"
alisema.
Aidha Sigala alionya viongozi wa ngazi za
vijiji na kata kutobweteka maofisini na badala yake kujikita katika kuhamasisha
wananchi katika shughuli mbalimbali za ukuaji wa uchumi kwa mtu mmoja au
vikundi kwa kuanzisha miradi endelevu itakayosaidia kuwaongezea kipato hususan
miradi ya maendeleoi ya kijiji.
"Viongozi ni wakati wa kutambua nini uhitaji wa
jamii katika maeneo yenu na si kubweteka bali ni kuhakikisha wa n a c h i wa n
a n u f a i k a na miradi mbalimbali ya maendeleo," alisema.
No comments:
Post a Comment