Na Heri Shaaban
IMEELEZWA kuwa wananchi wa Manispaa ya Ilala, Dar es
Salaam
wengi wanachelewa kupata huduma za afya mapema hadi
wanazidiwa
ndipo wanakumbuka kupelekwa vituo vya afya.
Hayo yalisemwa jana na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo,
Dkt.
Asha Mahita wakati wa uzinduzi wa zoezi la kampeni la
kutoa huduma
za afya kwa uwiano katika jamii Kata ya Gongolamboto.
Dkt. Mahita alisema, huduma hizo za kiafya ni muhimu
katika kusaidia
makundi maalumu ya watoto na wajawazito, wazee na
walemavu ndani
ya manispaa hiyo ili kukabiliana na changamoto hizo.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo, Jerry Silaa
alisema
wataalamu wanaeleza matatizo mengi ya kiafya hasa
magonjwa
yanayosumbua wananchi wengi yanatokana na uchafuzi wa
mazingira na
matumizi ya maji yasio salama.
Hata hivyo, aliwataka wananchi wake watumie utaratibu
huo wa kupata
huduma za uwiano bila malipo kwani ni muhimu na
utawasaidia watu
wenye kipato cha chini, wasio na uwezo kufuata huduma
hiyo karibu na
makazi yao.
No comments:
Post a Comment