IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya wajasiriamali nchini hawashiriki
mafunzo ya ujasiriamali hali inayopelekea wajasiriamali wengi kukosa ubunifu
zaidi katika shughuli zao, anaripoti Penina Malundo na Jazila Mrutu.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es
Salaam na mtafiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Utafiti wa Kisera katika
Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STIPRO), Bw. Musambya Mutambala wakati
akiwasilisha mada mbele ya wadau wajasiriamari.
Bw. Mutambala alisema kuwa kuna uhitaji
mkubwa wa kuwahamasisha wafanyabiashara wa d o g o wa d o g o k a t i k a
kuwaendeleza kupanua fikra zao ili waweze kukuza fikra zao katika kuongeza
ujuzi.
“Wajasiriamali wengi hawapo tayari kupata
mafunzo ya ujasiriamali sijajua ni kwa sababu gani kwani tunawahamasisha kila
siku juu ya ushiriki wao katika mafunzo hayo kwani yanawapa fursa ya kuongeza
ujuzi katika shughuli zao,”alisema Mutambala.
Ai d h a a l i s ema k a t i k a k u f a n
y a u t a f i t i w a k e aligundua kuna changamoto kubwa wanayokabiliana nayo
wajasiriamali wadogo wadogo ni pamoja na kukosa vitendea kazi hivyo ameiomba
Serikali kuwasaidia wajasiriamali hao kuweza kujikimu katika mahitaji yao.
“Katika
utafiti nilioufanya nimegundua kuwa wajasiriamali wengi wanashindwa kufanya
vizuri sababu ya vitendea kazi vyao vinakuwa vibovu na muda mwingi vinakuwa
vimepitwa na wakati hali inayopelekea vitu vyao kutokuwa vizuri,” alisema.
No comments:
Post a Comment