05 July 2013

LAPF YAWATAKA WAAJIRI KUWASILISHA MAFAO MAPEMA


Rehema Maigala na
Rachel Balama
MENEJA wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kanda ya kaskazini Amina Kassim, amewataka waajiri ambao wamejiunga na mfuko huo kuwasilisha mafao yao kwa wakati ili kuondoa usumbufu wa kufuatilia michango hiyo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara, Kassim amesema kama michango hiyo itawasilishwa kwa wakati itasaidia wanachama kulipwa mafao yao mapema mara baada ya kustaafu.
Alisema kuwa katika kuboresha huduma kwa wanachama wao LAPF ina mpango wa kuanzisha fao la elimu kwa lengo la kuwawezesha wanachama pamoja na familia zao.
"Tangu kuanzishwa kwa mfuko huu wa pensheni, tunatoa mafao sita ikiwa ni pamoja na msaada wa mazishi, ambapo sisi kama viongozi wa LAPF tumeamua kuanzisha fao jipya la elimu ambalo litamsaidia mwanachama pamoja na watoto wao," alisema Kassim.
Alisema kuwa lengo la kushiriki katika maonyesho hayo ni kutoa elimu kwa wanachama pamoja na kuelezea mafanikio waliyoyapata tangu kuanzishwa kwa mfuko huo.
A k i e l e z e a c h a n g amo t o zinazowakabili ni pamoja na wigo mfinyu kwa wanachama kujiunga na mfuko wa pensheni kutokana na uelewa mdogo.
Alisema LAPF imekuwa ikitoa riba nafuu na rahisi kwa wanachama wake hali ambayo imesababisha idadi ya wanachama kuongezeka siku hadi siku

No comments:

Post a Comment