Na Darlin Said
CHAMA cha Waandishi wa
Habari Wanawake (TAMWA) kimesema kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa
kijinsia katika jamii ya Watanzania hasa ubakaji bado ni tatizo linalohitaji
nguvu ya pamoja kulitokomeza. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa
chama hicho, Valerie Msoka alipokuwa akizindua ripoti ya utafiti wa unyanyasaji
wa kijinsia uliofanyika Aprili mwaka huu katika wilaya 10 za Tanzania bara na
Zanzibar.
Msoka alisema kwa mujibu wa utafiti huo imeonekana licha ya
vitendo hivyo kuendelea kuwepo, waathirika ambao ni wanawake na wasichana wengi
wao hawatoi taarifa kwa mamlaka husika ili hatua kali zichukuliwe dhidi ya
wahalifu. Alisema tabia ya kutotoa taarifa inasababishwa na mila na desturi
zilizowazunguka, hivyo alitoa wito kwa jamii kuachana na utamaduni wa kukaa
kimya pale wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Alisema uelewa wa jamii juu ya haki zao bado ni changamoto huku
umaskini ukiendelea kuwa kisingizio cha manyanyaso hayo hasa katika jamii ya
vijijini, hivyo alidai ni wajibu kwa Serikali kuhakikisha inawajengea uwezo
wakazi hao pamoja na kujenga miundombinu ya kutosha ili kuondoa kero
zinazosababisha uduni wa maisha ambao hutumika kama kigezo cha kuendelea kuwepo
kwa tatizo hili," alisema.
Awali alisema utafiti huo pia umebaini kuendelea kuwepo kwa ndoa
za utotoni hivyo ni vyema sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ikafanyiwa marekebisho
kwa lengo la kuzuia kuolewa msichana aliye chini ya umri wa miaka 18. Uzinduzi wa ripoti hiyo ni
mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa kujenga na kuimarisha usawa wa kijinsia
na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (GEWEII) unaoshirikisha
mashirika yanayotetea haki za jamii hasa wananwake na watoto yakiwemo TAMWA,
Jumuiya Wanawake Wanasheria Zanzibar (ZAFELA), Chama cha Wanasheria Wananwake
(TUWLA), Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Kituo cha Usuluhishi cha TAMWA
(CRC
No comments:
Post a Comment