26 July 2013

TFF KUTAFUTA SULUHISHO KWA NGASSA



 Na Ester Maongezi
KUTOKANA na utata wa usajili wa winga Mrisho Ngassa kati ya Simba na Yanga, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa lipo kwenye mkakati wa kulitafutia suluhisho tatizo hilo.Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah, alisema utata wa mchezaji huyo utashughulikiwa mara tu baada ya Kamati ya Sheria, Haki na Hadhi ya Wachezaji itakapokaa na kutatua mgogoro huo kwa kufuata kanuni.

"Utata wa Ngassa kama mchezaji unatatuliwa na kamati ya sheria ya wachezaji kwa hiyo kamati hiyo itakapokaa ndio itaweza kutoa uamuzi wa jambo hilo," alisema Osiah.Utata wa usajili wa mchezaji huyo umekuja mara baada ya Ngassa kutangaza kurejea Yanga mara tu baada ya Ligi kuu Tanzania Bara kumalizika ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo Wakati huohuo, klabu ya Simba imedai kuwahisha usajili wa winga huyo kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na kudai kuwa ni mchezaji wao wa halali na jina lake litakuwepo katika usajili wa wachezaji wao.

No comments:

Post a Comment